KAULI YA ALBERTO MSANDO KUHUSU SAKATA LA LEMUTUZ LILILOTIKISA MTANDAONI



From @albertomsando -Kaka na rafiki yangu @lemutuz_superbrandtz; Nimetamani sana nikae kimya upambane na ‘msala’ wako mwenyewe. Lakini nimeshindwa. Nimeshindwa kwa sababu naelewa na najua inavyokuwa pale unapopitia unachopitia. I have been there. Niseme kwamba kwa comments zote unaweza sasa kuelewa kiasi cha chuki dhidi yako. Kiasi cha furaha kwa maadui zako.
Lakini ndani yake usiache kuona kiasi kidogo cha upendo na huzuni kutoka kwa marafiki zako. Kosa lako ni kuruhusu kile ambacho wengi wanafanya kufika hadharani kwa kuwa karibu na kumpa nafasi aliyefikisha. Hilo ndio kosa lako la kwanza. “Kosa” la pili ni unavyoishi. Umeamua kuishi maisha yako vile ambavyo wewe mwenyewe umechagua. Kuna wengi wanakereka bila hata sababu.
Ni maisha yako! Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni kwamba unadhihakiwa, unadhalilishwa kwa sababu hiyo. HAYA NDIO MAMBO WENGI WANAYAPENDA NA KUFURAHIA. Sad. Ushauri wangu (unaweza ukawa wa kipuuzi na usio na maana) ni mwepesi. Endelea na maisha yako.
Pambana kuijenga Le Mutuz TV. Endelea kuelimisha na Straight Talks zako. Endelea kufurahia maisha. Usijibizane na wanaokutukana. Usiwashambulie wanaendelea kukudhalilisha. Fanya yale yanayokupendeza na kukufanya uwe bora zaidi. Na zaidi ya yote JIFUNZE kutokana na hili. Kumbuka nilichosema #ItCouldHaveBeenWorse #INGEWEZAKUWAMBAYAZAIDI.
Usimdhalilishe mtu yeyote hata kama ni adui yako mkubwa. Ukiweza picha na post ya Mange ifute. Usilipe ubaya kwa ubaya. Hakuna sababu ya kulifanyia marejeo tukio hilo. Kwa nafasi yako yapo mengi ya kuandikia sasa mfano, Uchaguzi mdogo, ujio wa Kagame na maana yake kwa Tanzania, kauli ya Trump dhidi ya waafrika na ukweli wake nk. nk. Kuna mengi ya kufanya.

Comments

Popular posts from this blog