BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARALA LA NNE
Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
==> Bofya Hapa Kuona ya Kidato cha Pili
==>Bofya Hapa Kuona ya Darasa la nne
Comments
Post a Comment