Kingunge Ataka Kujua Hali ya Tundu Lissu
Aliyekuwa
mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa (wa pili kushoto),
akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, wakimjulia hali Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Kigunge ameulizia hali ya Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa aliyekuwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhimbili.
“Vipi hali ya Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari), nimewauliza mimi tu niliyeng’atwa na mbwa mnanifanyia hivi, je Lissu mmemfanyaje maana majeraha yake yalikuwa makubwa?” amehoji Kingunge
Baada ya Mbowe kumueleza mkongwe huyo juu ya hali ya Tundu Lissu kwa sasa, alipata faraja na kusema ‘Aluta Continua’ ikimaanisha (kwa lugha ya Kireno) ‘Mapambano Yanaendelea’.
Comments
Post a Comment