Kumbe bila kuitwa na Waziri tusingejua Gigy ana mimba

Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa mjamzito na kuwashangaza wengi, amesema hakukusudia kuwajulisha watu bali ilikuwa kwa bahati mbaya wamejua

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv pia Gigy Money amewataka watu kumshukuru Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo Juliana Shonza kwa kumuita, kwani bila wito huo watu wasingemuona mtaani na kumuona akiwa na ujauzito wake.

“Kwanza Mumshukuru yule waziri la sivyo msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea bahati mbaya watu wakauona, alafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma mi nina undugu na serikali? Kama mtoto anaokotwa basi subirini nami wangu nitamuokota”, amesema gigy Money.

Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja siku chache baada ya watu kumuona na ujauzito, huku wengine wakidai ameweka mimba feki ili serikali imuonee huruma.

Comments

Popular posts from this blog