Posts

Breaking News: BOT yazifutia leseni Benki Tano

Image
 Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi. Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited. BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi. “Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.” “Ua

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI, WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA SAM KUTESA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. < Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ujumbe Maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiufungua na kuusoma Ujumbe huo maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa

NUNUA JIKO TUKUPELKEE HADI KWAKO BUREEE (DAR) NA ZAWADI YA MAFUTA BUREEEE

Image
Kwa Mara nyingine tena Bngo Deco Electronics, tunakuletea majiko makubwa ya kupikia kwa bei poa kabisa. Majiko haya yanadumu sana na yanakuja na warranty  ya mwaka mmoja, likisumbua tu tutakurekebishia. Nakwa kuthamini mchanngo wa Muungwana Blog kila mteja atakatoka katika Muungwana atapew dumu la mafuta ya alizeti BUREE na kama yupo Dar tutampelekea BUREE hadi kwake.   Kwa wateja wa mkoani gharama za kutuma jiko kwenda mkoani ni jukumu la mteja mwenyewe ila kama ni kumpelekea kwenye basi au lori la kuja mkoani basi tutatoa usairi BUREE hadi sehemu ya kutumia. Tupo Magomeni Mapipa mtaa wa Idrissa karibu kabisa na Butiama Restaurant.

NANDY ACHARUKA BAADA YA TAARIFA KUSAMBAA KUWA ANATOKA NA RUGE MUTAHABA.

Image
January 3, 2018 kumekuwepo na post kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msanii Nandy kudaiwa kutoka kimapenzi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Nandy ameamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Istagram kuhusu tuhuma hizo. Nandy Kupitia ukurasa wake wa Isntagram ameandika kuwa. “Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa. hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama uyo msambaza habari anavyo sambaza!” “Kwani suala la watu kusema na toka na boss wangu nalijua leo au nigeni kwangu sana mpaka nijiachie kwenda naye ma camp sijui ma club kama mnavosema???” – Nandy “Embu tuwe na utu please kwa hiyo me nimekuwa wakuja kiasi kwamba mshamba kiasi nikashindwa kujificha na mashungi juu basi kama ni hivyo  tumeshindwa kupishana kusafiri atangulie ndo nifuate,”– Nandy “Kwani sijui hata kama ingekuwa ni kwa nia nzuri  msingesema mnazani mambo ni marahisi kiasi hicho tupeane heshima kuna watu wengine hat

Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Aitwa Polisi

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo huku wakisema hawajui sababu ya wito huo. Wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha mbunge huyo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Sugu amesema leo Jumanne kuwa, juzi jioni alipigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba yeye na Masonga wafike jana ofisini kwa ajili ya mazungumzo lakini alimueleza kuwa itakuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa vigumu ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo. “Polisi walinipigia simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende Makao Makuu ya Polisi jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi. Sasa hivi tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini nadhani ni uchochezi,” amesema Sugu. Masonga amesema anaamini sa

Ikulu yatoa neno kuhusu kutokuapishwa kwa Dk. Slaa

Image
Balozi, Dk. Willibrod Slaa. WAKATI zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi. Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa. Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu. “Hili ni jambo ambalo siyo la kawaida, tumezoea mtu akiteuliwa kushika wadhifa fulani na rais baada ya siku chache, tunaona au kusikia kuwa ameapishwa, lakini kwa Dk Slaa ni zaidi ya mwezi sasa, kuna sababu zimetolewa? Tujulisheni,” ni moja kati ya simu nyingi za wasomaji wetu waliopiga chumba cha habari kutaka ufafanuzi. Kutokana na hali hiyo, Uwazi liliwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili kujua kwa nini imechukua muda mrefu kumuapisha Dk

SIWEMA AFUNGUKIA KUMUONA MWANAYE KWA NAY

Image
Nay wa Mitego akiwa na watoto wake. MZAZI mweza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amefungukia ishu ya kumuona mwanaye, Cartes kuwa, si kweli kwamba hajawahi kumuona tangu aondoke kwa jamaa huyo. Siwema mwenye maskani yake jijini Mwanza aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, si kweli kwamba hajawahi kuomuona mtoto wake kwani mara nyingi anapokwenda kumuona kwa mama wa mwanamuziki huyo, Nay anakuwa hajui. “Naongea naye kila mara, nimeshakwenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu,”   alisema Siwema.

Uchangudoa wa Zari Waibua Kimbembe!

Image
MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kukiri kuwa yeye ni changudoa mzee, kauli yake imeibua kimbembe. KUPITIA SNAPCHAT Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alitupia ujumbe akionesha kuwa yeye ni changudoa mzee, lakini mwenye mafanikio akimjibu hasimu wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto bila kumtaja. “Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+, mama uliyeachwa mara mbili na tuzo juu,” alisema Zari kupitia Snapchat. Kwa muda mrefu, Zari amekuwa kwenye tifu la aina yake baada ya Mobeto kuzaa na bwana wake, msanii wa Bongo Fleva miezi michache iliyopita. KIBEMBE KILIVYOIBUKA Kitendo cha Zari kutoa kauli hiyo, kimbembe kiliibuka mtandaoni mara baada ya ukurasa wa Instagram wa Global Publisher, kutupia habari hiyo ambapo wafausi wa mtandao huo walianza kurushiana maneno makali huku kila m

WATU 120 WAMEKAMATWA WAKIWEMO MAPADRI NCHINI DRC CONGO

Image
Zaidi ya Makanisa 150 yaliandamana nchini DRC Congo December 31, 2017 wakimtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani katika maandamano hayo imetolewa taarifa na Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Florence Marchal Katika taarifa iliyotolewa imesema watu saba wameuawa mjini Kinshasa na mmoja katika mkoa wa Kananga, katikati mwa Congo na kuongeza kuwa watu 82 wamekamatwa wakiwemo mapadri, katika mji mkuu Kinshasa, na 41 katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Katika hotuba yake ya kumaliza mwaka, Kabila amesisitiza kuwa kutangazwa  kwa ratiba ya uchaguzi wa December 2018, kumefungua njia ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Masoud Kipanya awatoa hofu Watanzania

Image
 KUFUATI taarifa kusambaa mitandaoni jioni ya leo Januari 1,2018 kwamba, mchora katuni maarufu Tanzania, Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi, Kipanya kupitia akaunti yake ya Twitter ameibuka na kuwatoa hofu Watanznia kwa kuandika kauli hii. “Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.” Taarifa hizo zinadai kuwa, Masoud Kipanya ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM, amekamatwa na Polisi baada ya kuchora katuni ambayo ina maudhi ya uchochezi kati ya wananchi na serikali. Aidha katika kauli yake Masoud hajaweka wazi iwapo amekamatwa na amepelekwa kituo kipi cha polisi na kama ameachiwa au bado.

Dk. Shika Atangaza Kuihama Tanzania, Anaelekea Wapi? Soma Hapa

Image
MAPYA TENA! Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo. Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani. “ Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa  Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York , nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR. “Hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, hizi

ELIMU YA BURE KWA WENYE MAGARI NA JINSI YA KUNUNUA MATAIRI YA GARI YAKO

Image
Hata kama huna gari kwa sasa naamini katika moja ya ndoto zako ni kumiliki gari, Isomee hii itakusaidia wewe na ndugu zako kama sio na rafiki zako. Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari lako).......Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE......hapo ndio inapotokea tairi mpya umenu

ALICHOKIANDIKA MKE WA KAFULILA BAADA YA KUONANA NA TUNDU LISSU LEO

Image
Leo December 30, 2017 Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Singida  Jesca Kishoa   alikuwa Nairobi Kenya ambapo alienda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake Dodoma na watu wasiojulikana. Kupitia account yake ya Instagram aliandika jumble usemao.>” Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000….. Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol. Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi.Glory to the Almighty God.Aluta Continua “

TRA Kumchunguza Kakobe Baada ya Kusema Ana Pesa Nyingi Kuliko Serikali

Image
Kufuatia Kauli ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepanga kumchunguza kiongozi huyo wa dini. Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; “Tupokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao “Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema. “Tunawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe tukaanza kupitia kumbukumbu zetu ili kuona namna Askof

EBITOKE TENA,AIBUKA NA MENGINE KUHUSU BEN POL,AFUNGUKA MENGI LIVE

Image
Mchekesha kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amefunguka uhusiano wake na msanii wa RnB Ben Pol ulivyo kwa sasa mara baada ya kupitia drama za hapa na pale. Ebitoke amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa licha ya kutofautiana hapo awali kwa sasa mapenzi yao yanaendelea kama kawaida. Hapana sijaachana naye, baada ya kulalamika kuwa hapokei simu yangu sasa hivi tupo vizuri kabisa, mlikuwa mnatuona hata kwenye baadhi ya show zake tupo pamoja, sasa hivi tupo fresh yeye ndiye boyfriend wangu sina mwingine,” alisema Ebitoke. Uhusiano wa wawili hawa ulianza June mwaka huu mara baada ya Ebitoke kujitokeza katika mitandao na vyombo vya habari na kudai kuwa anavutiwa na Ben Pol na angetamani kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi kitu ambacho kinaelezwa kilikuja kutimia hapo baadaye.

TCRA YASHUSHA GHARAMA ZA MAWASILIANO

Image
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018. Akitangaza punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza kutumika Januari Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi kufikia shilingi 2 mwaka 2022 Aidha Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.

Faida 10 za kutumia Mafuta ya Nazi

Image
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo: Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum. 2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula: Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo w