EBITOKE TENA,AIBUKA NA MENGINE KUHUSU BEN POL,AFUNGUKA MENGI LIVE


Mchekesha kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amefunguka uhusiano wake na msanii wa RnB Ben Pol ulivyo kwa sasa mara baada ya kupitia drama za hapa na pale. Ebitoke amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa licha ya kutofautiana hapo awali kwa sasa mapenzi yao yanaendelea kama kawaida.

Hapana sijaachana naye, baada ya kulalamika kuwa hapokei simu yangu sasa hivi tupo vizuri kabisa, mlikuwa mnatuona hata kwenye baadhi ya show zake tupo pamoja, sasa hivi tupo fresh yeye ndiye boyfriend wangu sina mwingine,” alisema Ebitoke.

Uhusiano wa wawili hawa ulianza June mwaka huu mara baada ya Ebitoke kujitokeza katika mitandao na vyombo vya habari na kudai kuwa anavutiwa na Ben Pol na angetamani kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi kitu ambacho kinaelezwa kilikuja kutimia hapo baadaye.

Comments

Popular posts from this blog