WATU 120 WAMEKAMATWA WAKIWEMO MAPADRI NCHINI DRC CONGO
Zaidi
ya Makanisa 150 yaliandamana nchini DRC Congo December 31, 2017
wakimtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani katika maandamano hayo
imetolewa taarifa na Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo
Florence Marchal
Katika
taarifa iliyotolewa imesema watu saba wameuawa mjini Kinshasa na mmoja
katika mkoa wa Kananga, katikati mwa Congo na kuongeza kuwa watu 82
wamekamatwa wakiwemo mapadri, katika mji mkuu Kinshasa, na 41 katika
maeneo mengine ya nchi hiyo.
Katika
hotuba yake ya kumaliza mwaka, Kabila amesisitiza kuwa kutangazwa kwa
ratiba ya uchaguzi wa December 2018, kumefungua njia ya maandalizi ya
uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment