TCRA YASHUSHA GHARAMA ZA MAWASILIANO
Mamlaka
ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha
gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika
moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018.
Akitangaza
punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza
kutumika Januari Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James
Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi
kufikia shilingi 2 mwaka 2022
Aidha
Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya
watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa
mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment