ELIMU YA BURE KWA WENYE MAGARI NA JINSI YA KUNUNUA MATAIRI YA GARI YAKO



Hata kama huna gari kwa sasa naamini katika moja ya ndoto zako ni kumiliki gari, Isomee hii itakusaidia wewe na ndugu zako kama sio na rafiki zako.
Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari lako).......Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote.
Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa.

Related image
Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE......hapo ndio inapotokea tairi mpya umenunua juzi kisha baada ya Wiki moja ya matumizi inapasuka puu ukiwa kwenye mwendo na kuanza kutafuta chanzo na usikione kuumbe lilisha Expire kitamboo......Chukua tahadhari rafiki yangu.
Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi Kama ifuatavyo.
CODE. SPIDI
F========80
G ========90
J ========100
K ========110
L ========120
M ========130
N ========140
P ========150
Q ========160
R ========170
S ========180
T ========190
H ========200
Huandikwa hivi
280/R/70/13/560/S
Hapo herufi S inawakilisha Spidi,180.

NINI MAONI YAKO?

Comments

Popular posts from this blog