Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde. Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde amesema kuwa si kweli kwamba serikali inaweza kuwaajiri wote kwenye sekta ya umma ila inachokifanya ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo ufugaji na biashara.Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Joseph Kenani lililohoji, serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa. Je, ni lini sasa serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani. “Katika azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hilo la vijana serikali, imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri wote kwenye sekta ya