Wakili Msomi Atinga Mahakamani Kudai Wanaume Wafutiwe Mahari

petee
Wakili msomi nchini Zimbabwe, Bi. Priccilar Vengesai ameanzisha kesi mahakamani ya kufutilia mbali mahari zinazotolewa na wanaume pale wanapooa akidai kuwa ni mila iliyopitwa na wakati.
Tokeo la picha la pete ya ndoa
Wakili huyo amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu nchini humo akitaka kusikilizwa kwa kesi yake huku akilalamika kuwa utamaduni huo unakiuka haki za kibinaadamu.
Bi. Priccilar Vengesai anaamini kuwa endapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinatakiwa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia.
Akizungumza na gazeti la serikali nchini Zimbabwe la Herald, Wakili huyo amesema kuwa anataka kuolewa upya baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika kwani hakuwa na sauti ya kuhoji kiasi cha mahari iliyotolewa na kujiona kama bidhaa.
“Nataka kuolewa tena sitaki kupitia kama niliyopitia kwenye ndoa yangu kwani sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mahari ilitolewa wala kujua hata ni kiasi gani.“amesema Bi. Vengesai na kuendelea kusimulia kisa hicho.
“Hali yote hiyo ilinifanya mimi kuonekana kama bidhaa ambapo kiwango cha thamani yangu kilipendekezwa na wajomba zangu na mume wangu akalipa. Hatua hiyo ilinivunja moyo kwani ilinifanya nijione mnyonge mbele ya mume wangu na kujihisi kama nimenunuliwa.“amesema Wakili huyo.
Hata hivyo, Bi. Vengesai ambaye anatoka katika kabila la washona amesema kuwa anatamani kuingia kwenye ndoa mapema baada ya mahakama kutoa tamko juu ya madai yake.
Nchini Zimbabwe mahari hutolewa na upande wa familia ya mwanaume na kama haitatoka basi mwanamke hataruhusiwa kuishi na mwanamme kwa namna yoyote ile

Comments

Popular posts from this blog