ZARI THE BOSS LADY AUMBULIWA NA MITANDAO YA HABARI NCHINI UGANDA!MAISHA YAKE YA MTANDAONI NA NYUMBANI KWAO MAZITO YAIBUKA

Mwanamama Zarinah Hassan Tlale almaarufu Zari The Boss Lady.
Wakati akitajwa kuwa mmoja wa wanawake masta-watafutaji na matajiri wa Afrika Mashariki, mwanamama Zarinah Hassan Tlale almaarufu Zari The Boss Lady ameumbuliwa, Risasi Jumamosi limetonywa.
KIJIJINI MAMBO SI MAMBO
Zari anadaiwa kuumbuliwa na mitandao ya habari za mastaa ya nchini Uganda ambayo imeeleza kwamba, pamoja na kuwa na fedha nyingi na maisha ya kufuru, lakini huko nyumbani au kijijini kwao, Jinja nchini Uganda mambo si mambo.
Akiwa na watoto wake.
Kwa mujibu wa mitandao hiyo iliyoamua kumwanika Zari baada ya kutajwa kuwa na utajiri mkubwa miongoni mwa mastaa wa nchini humo, Jinja ndiko alikozaliwa na kukulia kabla ya kuhamia Kampala, lakini maisha ya ndugu zake hasa makazi ni duni au ya hali ya chini ukilinganisha na mbwembwe za utajiri wake.
WATU WANASHANGAA
“Kwa tunaofahamu kijijini kwao (Jinja), tunashangaa kama kweli ana utajiri kama anavyojinadi maana maisha ya ndugu zake ni ya chini. Hata nyumba ya bibi yake na ndugu zake hazina hadhi ya yeye kujiita Boss Lady. “Inawezekana kweli ana utajiri mkubwa wa fedha, majumba na magari ya kifahari huko Kampala na Afrika Kusini. “Tumemuona mara kadhaa akinadi majumba yake ya ghorofa na hoteli zake za Munyonyo (Kampala).
MAJUMBA YAKE SAUZ
“Pia majumba yake ya Pretoria na Johannesburg huko Afrika Kusini (Sauz) aliyoachiwa na marehemu mumewe, Ivan Ssemwanga na ile aliyonunuliwa na mpenzi wake wa sasa ambaye ni msanii wa Bongo Fleva.
“Pia ukimuona Zari akiposti mapicha akiwa na yale magari yake ya kifahari kama Hummer H2, Ferrari, Lamborghini, Mercedes Benz na mengineyo, ukioneshwa nyumbani kwao kule Jinja unaweza kubisha, lakini ukweli ndiyo huo,” ulieleza mtandao mmoja na kuongeza: “Kiukweli kwa fedha alizonazo, Zari alipaswa kupajenga kwao maana ndipo nyumbani kwao, ndipo asili yake na mwacha asili ni mtumwa, hatuandiki kwa ubaya ila tunafanya hivi kumkumbusha kwao apajenge napo paendane na hadhi yake kama anavyopenda kujiweka aonekane ‘high class’.
“Tunachofahamu ni kwamba, mama mzazi wa Zari (Fatuma Hassan) aliolewa na baba yake Zari huko Jinja, lakini kadiri muda ulivyosonga, wazazi wa Zari walitengana ambapo mama Zari alipitia mambo mengi sana katika kuwalea wanaye nane akiwemo Zari wakiishi maisha magumu ya kijijini kule Jinja. “Baadaye mama Zari alihamia na kuanzisha maisha mapya jijini Kampala akiwa na bintiye Zari.
“Ndicho kipindi ambacho Zari alianza kutembea na wanaume wenye fedha ambapo alifanikiwa kuolewa na Ivan ndipo akamjengea mama yake ile nyumba ya ghorofa iliyopo
Munyonyo (Kampala).
UTAJIRI WA ZARI
Zari ambaye amepewa jina la Boss Lady kutokana na utajiri wake anaelezwa kuwa anamiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala nchini Uganda, vyuo vya urembo na maduka ya vipodozi nchini Afrika Kusini alivyoachiwa na mumewe ambavyo vimekuwa vikimuingizia mkwanja mrefu.
Pia Zari ni muandaaji wa shoo zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya hivyo kuaminika kuwa ana uwezo wa kupajenga kwao na kupafanya kuwa na hadhi inayoendana na jina lake.
SI ZARI TU Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba, si Zari tu anayekumbwa na ishu hiyo ya kutojenga vijijini mwao bali kuna wimbi la vijana wengi ambao mjini wanaonekana kuwa na maisha bora lakini ukifika vijijini mwao walikozaliwa ni aibu tupu.
Na MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi

Comments

Popular posts from this blog