Mwanamfalme Wa Saudi Arabia Afariki Katika Ajali Ya Ndege

MWANA wa mfalme  nchini Saudi, Arabia Mansour bin Muqrin,  amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na Yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Mwana mfalme huyo,  Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri  na maofisa kadhaa wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, kituo cha runinga ya Al-Ikhbariya imesema.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika hadi sasa.
Kuna habari kwamba Saudi Arabia ilkuwa imetungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.
Pia, wakati wa wikiendi, watu wengi wakiwemo wana wa wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.  Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi, Mohammed bin Salman.
Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.  Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadhaa baada yake kurithi ufalme wa nchi hiyo mwaka 2015.
Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.
CREDIT: BBC SWAHILI

Comments

Popular posts from this blog