Meya wa Jiji la Mwanza Akamatwa na Polisi
TAARIFA zilizotufikia kwenye dawati letu la habari zinaeleza kuwa, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi huku ikidaiwa kuwa amri ya kukamatwa kwake ni agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella.
Hayo yamesemwa na Mariam Lima ambaye
ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na Meya Bwire
ambaye ameeleza kuwa kuwekwa kwake sentro ni kunatokana na agizo la
mkuu wa mkoa.
Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru
kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
cha Jiji la Mwanza.
“Nimepata taarifa za meya kuwekwa
mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema
Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017.
Taarifa zinasema meya Bwire
amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John
Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo.
Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.”
Tangu Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa
Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro kila upande
ukiutuhumu mwingine kuhujumu shughuli za maendeleo.
Updates:Meya Bwire ameachiwa kwa dhamana kwa madai ya kutaka kufanya kitu kibaya kwenye msafara wa Rais Magufuli.
Comments
Post a Comment