Rais Magufuli Anastahili Pongezi, Amefunua Blanketi Lililotufunika
Rais Dk. John Pombe Magufuli. M UNGU ni mwema kwa sababu ametufikisha leo tukiwa wazima, hakika ahimidiwe daima. Leo nachukua nafasi hii kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa mafanikio aliyotuletea ndani ya miaka miwili ya utawala wake. Ninapofanya tathmini ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli, ni kama narudia kwa sababu juzi na jana wengine wameandika au kusema kupitia vyombo vya habari. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 na Rais Magufuli kuibuka mshindi, alianza kuonesha kwa haraka kuwa yeye ni kiongozi asiyetaka mchezo kwenye kazi. Aliliambia taifa kuwa alipokea nchi ikiwa imejaa uozo kila idara na alitumia hoja hiyo kukataa hoja ya kupendekezwa kwa Katiba Mpya, iliyowahi kutolewa na baadhi ya watu wakati alipotimiza mwaka mmoja madarakani kwa kusema wazi, ‘niacheni niisafishe nchi kwanza.’ Mwaka wake wa kwanza alifanya mengi yaliyowafurahisha wananchi wengi, kama vile kufuta safari za nje kwa maofisa wa serikali labda kama ni za lazima s...