Waziri Wa Tamisemi Atoa Maagizo 6 Kwa Wakuu Wa Mikoa
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo. Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba. Waziri Jafo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo, ameeleza kwamba jumla ya watahiniwa 909,950 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 662,035 wamefauli kwa daraja A – C ikiwa ni sawa na 72.76% ya watahiniwa wote. Kufuatia ufaulu mkubwa uliojitokeza ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikalli za Mitaa, imetoa maelekezo kwa mikoa yote ili waweze kuanza maandalizi mapema ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema mwakani kabla ya kukamilika kwa uchaguzi wa wanafunzi hao. Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mitihani wanapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza Januari 2018, maelekezo yafuatayo yametolewa. 1. Wakuu wa Mikoa yote wametakiwa kuhakikisha kuwa miundo