Posts

MKUU WA WILAYA YA MBULU,ATATUA MGOGORO WA KIMPAKA KATI YA MBULU NA BABATI.

Image
Mkuu wa wilaya ya Mbulu C helestino S. M ofuga jana tarehe 10/10/2017 ametatua mgogoro wa kimpaka kati ya wilaya ya Mbulu na babati ,ambako kulitokea machafuko usiku wa kuamkia jana na kusababisha kubomolewa kwa nyumba mbili.  Mgogoro huo wa Siku ulishatatuliwa na kamati za ulinzi na usalama za babati na Mbulu mnamo mwezi wa sita. Wakuu wa wilaya babati Raymondi mushi na C helestino S. Mofuga walitatua mgogoro huo baada ya kutuma watalaam kutafsiri mipaka ya wilaya hizo Mbulu.  Hata hivyo mgogoro huo uliibuka tena Jana baada ya wananchi kubomoa nyumba mbili kwa madai zimejengwa katika maeneo ya malisho.  Mkuu huyo  wa wilaya ya mbulu amekemea vikali t a bia za kuharibu Mali za watu wengine na kuwaagiza wote waliobomolewa kuripoti kwa mkuu wa wilaya ya babati kwa kuwa wapo babati kiutawala, ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahalifu.  Pia mkuu wa wilaya ameagiza viongozi kusimamia mipaka kikamilifu ili kuepusha machafuko yasitokee.

BAMIA Husaidia Wagonjwa wa Vidonda vya Tumbo.

Image
Watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia. Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali? Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na beta carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona. Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini. Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta. Husaidia pia kulainisha choo. Vilevile ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza. Wataalamu wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo. Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa

Mtoto wa Mwalimu Mkuu Aanika Alivyomkuta Baba Yake Amejinyonga

Image
MTOTO Frank Benedicto (14) ni mtoto mkubwa wa Mkuu wa Sekondari ya Migukulama, Benedicto Lweikiza (45) aliyejinyonga juzi, amesema alitahamaki kumkuta baba yake akiwa amening’inia darini. Lweikiza alijinyonga hadi kufariki juzi saa tisa alasiri katika mtaa wa Kilabela Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Mwalimu huyo alikuwa anafundisha Sekondari ya Migukulama iliyopo Kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema. Mtoto wa marehemu huyo aliyekuwa akiishi na baba yake kwenye nyumba hiyo, anasoma kidato cha kwanza katika Sekondari ya Sima iliyopo wilayani hapo, alisema baada ya kutoka shuleni alikuta mlango wa nyumba yao upo wazi hivyo akadhani baba yake atakuwa kwa majirani. “Asubuhi niliagana vizuri na baba yangu wakati nikienda shuleni, jioni niliporudi ndipo nikakuta baba amejinyonga juu ya dari na kabla sijagundua kitu chochote nilikuta mlango wa nyumba upo wazi nikadhani yupo kwa majirani nilipoingia chumbani sikuamini nilichokiona

Majambazi Walivyomtwangwa Risasi Mwenzao Mbele ya Polisi

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah. ROBERT Massawe (51) , mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake. Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58. Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issa h imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo. Alisema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki. Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam. Kamanda Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufa

Chadema Yapata Pigo Lingine

Image
Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA. Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli. “Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao na hii ndio mikakati yetu” alisema Rubeya. Rubeya aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi. “CCM ndio chama tawa

WEMA SEPETU AMSHUKIA VIKALI SOUD BROWN,AMPA MAKAVU IKISA MAMA YAKE

Image
     There is Limits to everything jamani… Sipendi kabisa wen people involve my Mother kwenye mambo ambayo hata hayamuhusu… Niachie mama angu Soudy… I dont like it wen u bother her like dat only for u to record her alafu uje kumuanika like this… Hivi kwani @soudybrown huna mama wa kumfanyia hivyo unavyofanya… Sasa basi jus like da way huwezi mfanyia mama ako basi usiwafanyie na mama wa wenzako… Have some Respect atleast… Like I said kuna limits katika kila kitu… Hayo mambo yako ya Shilawadu yabaki huku kwetu vijana.. Wazazi tuwaache kama walivyo… Umenikera sana kwakweli… Sijapenda hata kidogo.

TANGAZO: VIWANJA VINAUZWA DODOMA MJINI

Image
Viwanja vinauzwa vipo Dodoma maeneo ya Mnada wa zamani njia ya kwenda Kondoa, SQ.M 1 ni 15,000... Ni kilometa 5 kutoka Jamatini. piga simu hii kwa maelezo zaidi.  0754461753

DIAMOND PLATINUMZ NA RICK ROSS WAKINUKISHA,BABU TALEE ASHUHUDIA LIVE

Image
          Meneja @babutale @richforever na @diamondplatnumz wakielekezana Kitu Flani #location #MiamiUSA ras_vegaHatariii mnyamaaa amekutana na mnyamaaa unyamani  

Mifupa ya Binadamu Yakutwa Kwenye Bwawa Mkoani Shinyanga

Image
KAMANDA wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga. Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule alidai kuwa iku ya Jumatatu  watu walipoona viungo hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao walifika na kukuta viungo hivyo. “Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne. “Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu  “Katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu,” alisema Simon Haule. Aidha Kamanda Haule alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo

ALI KIBA NA MANGE KIMAMBI MAPYA YAIBUKA

Image
              Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Seduce me’ amefunguka na kusema kuwa Tanzania kila mtu ana haki na uhuru wake hivyo hata yeye anajisikia vizuri kuona watu maarufu wanapenda kazi zake na kudai ana haki ya kupendwa na Mange Kimambi Alikiba amedai kuwa Mange Kimambi ni moja kati ya mashabiki zake na kusema anashukuru sana kuona anapenda kazi zake na kumpa nguvu katika kazi zake hizo kwa kutoa ‘support’. Ni kama shabiki wangu na ‘appreciate’ anapenda muziki wangu kwa sababu mimi namuheshimu kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anani ‘support’ kwenye kazi zangu lakini pia kutokana na uhuru hivyo kila mtu ana haki na vilevile mimi nina haki ya kupendwa na mtu yoyote yule, hivyo nina haki ya kupendwa na Mange Kimambi pia” alisema Alikiba Mbali na hilo Alikiba alisema anajisikia vizuri kuona muziki wake unazidi kufika mbali zaidi duniani na kuendelea kufanya vizuri nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla. “Najisikia f

Breaking News: Raila Odinga Ajiondoa Kwenye Uchaguzi Mkuu Kenya

Image
Raila Odinga Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao unapangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu. Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu. Bw. Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia ili nzuri.

Nafasi Za Kazi Chuo Kikuu Cha Arusha

Image
The University of Arusha, a Chartered Seventh-day Adventist institution of higher learning situated about 30 km from Arusha city, off the Arusha-Moshi highway, is seeking to recruit a suitably qualified individual to fill, with immediate effect, a vacant position in the Directorate of Finance. JOB TITLE: DIRECTOR OF FINANCE AND ACCOUNTING (DFA) The Director of Finance and Accounting (DFA) of the University shall be appointed by the University Council in consultation with the Vice Chancellor and the Chair of Finance and Development Committee of the Council. (a) Qualifications Holder of full Accountancy qualification and must be registered with NBAA as Certified Public Accountant i.e. CPA (T), ACCA, ACA or equivalent plus at least 5 years work experience in a similar position. (b) Remuneration This will depend on whether the person recruited is employed on church terms or on fixed-term contract terms. Nevertheless, an attractive package awaits the right candidate f

Nafasi za Kazi Meru University

Image
Meru University of Science and Technology (MUST) wishes to recruit qualified and dedicated staff to fill the following vacant positions. ACADEMIC POSITIONS PROFESSORS – GRADE 15 – MUST/ACA/01/17 (1 POST IN EACH CATEGORY) Applicants are invited for post of Professor in the following areas:- Food Science Human Nutrition and Dietetics Plant Breeder Agricultural Economics Business Management Economics Procurement & Logistics Computer Science Computer Security and Forensics Artificial Intelligence Information/Library Science Mechanical Engineering Civil Engineering Electrical/Electronics Engineering Biosystems Engineering Architecture Health Systems Management Public Health/Environmental Health Community Health Clinical Medicine Health Records and Information Management Nursing Applied Statistics Theoretical Physics Actuarial Science Nuclear Physics Material Science Electronics Geophysics Organic Chemistry Industrial Chemistry Physical Chemistry

Nafasi Ya Kazi: Mkuu wa Chuo cha KIITEC Arusha

Image
The Principal serves as the Chief Executive Officer of the Institute and provides a clear focus on all matters related to the effective leadership and management of teaching, learning and quality to achieve academic excellence for the Institute. As KIITEC is growing in Tanzania as a center of excellence in East Africa and is scheduled to be duplicated in other sites, the Principal position will become a key role for our strategy implementation. Location Other Arusha District Arusha Description REPORTS TO: The Board of Directors SUPERVISES: Teachers, General staff and Students of the Institute SPECIFIC DUTIES: The KIITEC Principal shall: · Manage, and supervise effectively the operation of the Institute in harmony with the vision, mission, values and goals of the Institute · Supervise the overall financial status of the Institute · Build strong collaborative links with other academic institutions, stakeholders and donors within and outside Tanzania · I

Wivu wa Mapenzi Wasababisha Mauaji ya Kinyama ya Watu wawili

Image
Watu wawili wamefariki dunia na mwingine mmoja kujijeruhi baada ya kutokea ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi mjni Bunda. Tukio hilo lilitokea jana saa tano asubuhi katika Mtaa wa Bunda Stoo baada ya mtu mmoja kuwavamia watu wawili kisha kuwachoma visu kabla ya kujichoma mwenyewe. Akizungumza mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed alisema jana kuwa waliouawa ni Daudi Phares (29) mkazi wa Bunda na msichana aliyetambulika kwa jina moja la Monica (22) mkazi wa Magu mkoani Mwanza. Kamanda huyo alimtaja aliyejijeruhi baada ya kujichoma kisu maeneo mbalimbali mwilini mwake kuwa ni Selemani Jeremia (33) ambaye ni mkazi wa Magu. Alisema kuwa siku ya tukio Selemani alisafiri kutoka Magu mkoani Mwanza hadi Bunda ambapo alifika nyumbani kwa Daudi na kumkuta akiwa na Monica. Baada ya kufika nyumbani hapo Selemani alianza kumchoma visu Dauidi katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kifuani upande wa kushoto na kusababisha ki

MKUU WA WILAYA YA MBULU AAGIZA KITUO CHA POLISI KUJENGWA HARAKA.

Image
Mkuu Wa wilaya ya mbulu  chelestino s mofuga leo 09/10/2017 amekutana na wajumbe wa WDC  wa kata ya Eshkesh , kujadili maendeleo ya kituo cha polisi cha yaeda chini ambacho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba 2017.  Mkuu huyo amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi kuwachukua maelezo na  kuahidi kusimamia kikamilifu  michango ya wananchi ili kujenga kituo hicho.  Mkuu wa wilaya aliunda tume kuchunguza matukio ya ujangili wa nyara za serikali, wizi wa mifugo na mauaji ya binadamu mnamo mwezi wa nne 2017, na moja ya mapendekezo ya uthibiti wa matukio ya uhalifu ni kujenga kituo cha polisi. Wajumbe hao wamebainika kusuasua kusimamia michango licha ya wananchi kuunga mkono ujenzi huo. Mkuu wa wilaya ametoa siku 30 kukamilisha michango ya ujenI wa kituo cha polisi.

Waziri wa afya afariki baada ya kukimbia

Image
Slim Chaker aliteuliwa waziri wa afya mwezi uliopita Waziri wa afya nchini Tunisia amefariki kutokana na mshutuko wa moyo baada ya kushiriki katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa saratani. Slim Chaker, 56, aliugua baada ya kukimbia mita 500, kufariki kwenye hospitali ya kijeshi, kwa mujibu wa wizara ya afya. Waziri mkuu Youssef Chahed alisema kuwa amempoteza ndugu ambaye alikuwa akitoa huduma ya kibinadamu. Wanawake waislamu nchini Tunisia waruhusiwa kuolewa na wanaume wasio waislamu Mbio hizo ziliandaliwa kwenye mji wa pwani wa Nabeul siku ya Jumapili kuchangisha fedha za kujenga zahanati ya watoto ya kutibu ugonjwa wa saratani. Bwana Chaker aliteuliwa kuwa waziri wa afya mwezi uliopita wakati wa mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.

Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Kimataifa Yatikisa Uingereza

Image
                Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha. Baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya nchini Uingereza. Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ . Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA ,GARI YA ABIRIA AINA YA HIECE LATUMBUKIA ZIWANI

Image
              Gari ndogo la abiria (hiace) likiwa na abiria limetumbukia ziwani wakati likijaribu kuingia kwenye kivuko cha Kigongo Ferry jijini Mwanza, watu watatu tu mpaka sasa wameokolewa Chanzo: Radio Free Afrika

SHAMSA FORD AZIDI KUMSHUKIA ILALA MJINGA,AMPA MAKAVU LIVE

Image
          UKITAKA kujua kichaa cha ‘Queen’ wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, basi jaribu kuichokonoa ndoa yake, na hicho ndicho anachokifanya mtu mmoja aliyemfahamu kwa jina la Ilala Mjinga, ambaye kazi yake ni moja tu, kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuhusiana na ndoa yake na mumewe, Chid Mapenzi. Kwa mujibu wa Shamsa ambaye siku chache nyuma alisema kuwa anamuona jini-mkatakamba anainyapianyapia ndoa yake, hatimaye mambo yakamfika shingoni na kuamua kushusha waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiwataka wale wote ambao wanadhani atakuja kuachana na mumewe, basi wajue kwamba hiyo ni ndoto sawa na kusubiri embe dodo kwenye mti wa korosho! NA ISRI MOHAMED/GPL Post Views: 22