MKUU WA WILAYA YA MBULU,ATATUA MGOGORO WA KIMPAKA KATI YA MBULU NA BABATI.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino S. Mofuga jana tarehe 10/10/2017 ametatua mgogoro wa kimpaka kati ya wilaya ya Mbulu na babati ,ambako kulitokea machafuko usiku wa kuamkia jana na kusababisha kubomolewa kwa nyumba mbili.
Mgogoro huo wa Siku ulishatatuliwa na kamati za ulinzi na usalama za babati na Mbulu mnamo mwezi wa sita. Wakuu wa wilaya babati Raymondi mushi na Chelestino S. Mofuga walitatua mgogoro huo baada ya kutuma watalaam kutafsiri mipaka ya wilaya hizo Mbulu.
Hata hivyo mgogoro huo uliibuka tena Jana baada ya wananchi kubomoa nyumba mbili kwa madai zimejengwa katika maeneo ya malisho.
Mkuu huyo wa wilaya ya mbulu amekemea vikali tabia za kuharibu Mali za watu wengine na kuwaagiza wote waliobomolewa kuripoti kwa mkuu wa wilaya ya babati kwa kuwa wapo babati kiutawala, ili hatua zichukuliwe dhidi ya wahalifu.
Pia mkuu wa wilaya ameagiza viongozi kusimamia mipaka kikamilifu ili kuepusha machafuko yasitokee.
Comments
Post a Comment