Posts

Kanisa la Askofu Gwajima labomolewa

Image
Dar es Salaam. Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Mbezi Inn linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima limebomolewa. Nyumba hiyo ya ibada ambayo pia ilikuwa ikitumika kama kituo cha maombezi imebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads). Imeelezwa kanisa hilo limejengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro ya mita 121.5. Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, pia limekuwa likitumika  kama kituo cha kufundishia wachungaji limebomolewa jana jioni hali iliyosababisha waumini wa Kanisa hilo kusalia nje. Mwananchi imefika katika kanisa hilo na kukuta  vitu vikiwa nje na baadhi ya waumini wakiendelea  na maombi nje. Mmoja wa waumini ambaye hakutaka kujitambulisha kwa madai si msemaji, amesema kanisa leo limebomolewa lakini injili inaendelea kuhubiriwa kama kawaida . "Tunaendelea na huduma na kesho tutakuwa na ibada itakayoanza saa kumi jioni "amesema. Muumini mwingine pia amesema hali ilikuwa mbaya jana wakati kanisa hilo linabomolewa kwani wali

Kauli ya Rais Magufuli Baada ya Kupata Taarifa za Lissu

Image
RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake kutokana na kushambuliwa kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema). “Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” amesema Rais Magufuli. Stori zinazo husiana na ulizosoma

BREAKING: Tundu Lissu Apigwa Risasi

Image
MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano. Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa kwenye gari kisha kumpiga risasi za miguuni na tumboni. Imeelezwa kuwa alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.  Dereva wake akiwa ameshika nguo na viatu vya Tundu Lissu Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana. Gari la Mbunge Lissu likionekana na baadhi ya matundu zilipopigwa Risasi  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji. "Hli ya Tundu Lisu ni mbaya Sana

Kutajwa Sakata la Madini… Waziri Simbachawene, Ngonyani Wajiuzulu

Image
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene. WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa hizo ili kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika kwa ubadhilifu kwenye Ripoti za Uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite. Uamuzi a viongozi hao umekuja ikiwa ni dakika chache baada ya Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya usalama. Kwa upande wake, akiongea na Mwananchi leo Alhamisi mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo. Naibu Waziri w

Breaking News: Mtekaji Wa Watoto Arusha Auawa Kwa Kupigwa Risasi

Image
Mtuhumiwa Samson Petro enzi za uhai wake. Kijana aliyehusika na matukio ya utekaji watoto mkoani Arusha, Samson Petro (18) amefariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho alipozungumza na waandishi wa habari. Kamanda Mkumbo amesema kijana huyo ambaye alikamatwa mkoani Geita alikokuwa amekimbia kabla ya kurejeshwa Arusha alitaka kukimbia alipokuwa anakwenda kuwaonyesha polisi watuhumiwa wenzake wa utekaji  saa tano usiku wa jana Jumatano. Hivi karibuni alipokamatwa mkoani Geita, kijana huyo ambaye sasa ni marehemu alikiri kuwateka watoto wanne mkoani Arusha baada ya kukamatwa mjini Katoro wilayani Geita alikotekeleza tukio lingine la utekaji. Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi wiki iliyopita, kijana huyo alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000. Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha w

Hashim Rungwe Ashikiliwa na Polisi Dar

Image
Hashim Rungwe Spunda. ALIYEKUWA mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe Spunda anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku nne sasa. Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akituhumiwa kughushi nyaraka. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne. Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.

DENTI ACHARANGA WATU VISU MTAANI!

Image
Paulo Ndensai akiuguza majeraha. MWANAFUNZI wa kidato cha pili katika shule moja ya sekondari Wilaya ya Kinondoni jijini, Samuel Wilson, Jumanne iliyopita, saa mbili usiku, alifunga mtaa maeneo ya Mwenge Mlalakuwa na kuwachoma visu watu kadhaa akiwemo Paulo Ndensai na Yasin Mohammed. Akisimulia kwa uchungu tukio hilo mmoja wa mashuhuda alisema mwanafunzi huyo alikuwa akimpiga kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mohammed huku akimchoma kwa kisu alichoshika hali iliyowafanya wananchi waliokusanyika eneo hilo kukimbia kwa kuhofia usalama wao. Shuhuda huyo alisema denti huyo akiendelea kumshambulia Mohammed ambapo chanzo cha ugomvi huo hakijawekwa bayana, kaka yake Mohammed aitwae Paulo Ndensai alitokea na kwenda kumuokoa mdogo wake. “Katika harakati za kumuokoa mdogo wake, mtuhumiwa alimuacha aliyekuwa akimshambulia na kuhamishia varangati kwa kaka mtu ambapo alimchoma kwa kisu kichwani juu kidogo ya sikio la kushoto, kingine akamchoma kichwani juu, hali

RAILA ODINGA AMWITA KIBA KENYA, ATUMIWA NDEGE BINAFSI

Image
Alikiba. DAR ES SALAAM: Upepo mwanana bado unaendelea kumpuliza, staa namba moja wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ baada ya mgombea anayewakilisha Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Omolo Odinga, kudaiwa kumuita nchini humo. Kwa mujibu wa chanzo kisicho na chembe ya shaka, Kiba anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Seduce Me, alipata mwaliko huo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni saa chache mara baada ya Odinga kushinda kesi ya uchaguzi Katika Mahakama ya Juu aliyokuwa amemfungulia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye mambo yalimuwia mazito. Kenyatta alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IBEC) katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Agosti 8, mwaka huu ambapo Odinga alifungua kesi hiyo mahakamani. Baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, iliufuta uchaguzi huo kwa kueleza kuwa tume ya uchaguzi haikuzingatia uadilifu. ODINGA KICHEKO Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakaman

BREAKING: Wabunge wa Upinzani watoka nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Ukawa wasusia na kutoka nje shughuli ya kuapishwa kwa wabunge wa viti maalum 7 wa CUF. Wabunge hao ni wale waliopatikana baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho Prof Lipumba kutangaza kuwavua uanachama Wabunge 8 wa chama waliokuwepo kwasababu mbalimbali ikiwemo ya maadili.

RIPOTI YA MAKINIKIA ALMASI, TANZANITE BUNGENI KESHO

Image
             WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, kesho anatarajiwa kukabidhiwa taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 kuhusu na makinikia ya almasi na biashara ya madini ya tanzanite. Kwa mujibu wa taarifa za bunge hafla fupi ya makabidhiano hayo itafanyika katika viwanja vya bunge na viongozi wa kitaifa watakuwepo. Kabla ya Waziri Mkuu kukabidhiwa taarifa hizo, kamati hizo mbili zitakabidhi taarifa zake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye atakabidhi kwa Waziri Mkuu. Taarifa hizo mbili zinazosubiriwa kwa makini hasa baada ya taarifa za kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuibua makubwa katika makinikia kwenye makontena bandarini. Kamati hizo maalumu zote zilikuwa na idadi sawa ya wabunge ambao ni tisa na zililenga kushauri juu ya mfumo bora wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya almasi na Tanzanite hapa nchini. Kamati iliyohusu almasi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu

HAMISA MOBETO KUZAA NA BWANAKE… ZARI THE BOSS LADY ATINGA BONGO KUPATA UKWELI

Image
                      Zarina Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ . BAADA ya maneno mengi kusemwa Bongo kufuatia madai ya bwana’ke kuzaa na mwanamitindo mwenye jina kubwa, Hamisa Hassan Mobetto, mwanamama mjasiriamali mwenye jina kubwa Afrika Mashariki, Zarina Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’ anadaiwa kuendelea kuliamsha dude baada ya kutinga Bongo na kuanza kudodosa ili kupata ukweli wa ishu hiyo. Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni makini, awali Zari alitinga Bongo mapema wiki iliyopita na kupigwa chabo na ‘wadakuz’ AKIWA KATakiwa nyumbani kwa jamaa huyo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva huko Madale jijini Dar. Akiwa katika pozi. Ilidaiwa kwamba, hata hivyo, hakukaa sana kwani aliondoka kwenda kwenye kumbukumbu ya siku 40 za kifo cha mama yake, Halima Hassan nchini Uganda kabla ya kurejea Bongo wikiendi iliyopita.             Kwa taarifa yenu Zari amejaa tele Bongo na lengo lake ni kuchimba na kupata ukweli juu ya madai ya Hamisa kuzaa na bwana’ke.Unajua akiwa

Polisi wamkamata Mtekaji Watoto

Image
POLISI mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Mkoa wa Arusha wamemtia mbaroni mtuhumiwa wa utekaji watoto akiwa na mtoto mwenye umri wa miaka miwili katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu, Katoro Wilaya na Mkoa Geita aliyekuwa akimshikilia akidai apewe Sh milioni nne. Samson Peter amekamatwa usiku wa kuamkia jana baada ya timu maalumu ya Polisi ya askari tisa, watano kutoka Arusha wakiongozwa na Mkaguzi wa Polisi Amani na wa Geita askari wanne wakiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, James, kuizingira nyumba ya wageni aliyokuwa amejificha mtuhumiwa na mtoto aliyemteka tangu Septemba Mosi. Akithibitisha hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema mtuhumiwa alikamatwa saa mbili usiku juzi katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Shitungulu katika Mtaa wa California, Kata ya Katoro wilayani Geita akiwa chumba namba 11 na mtoto huyo Justine Ombeni (2) aliyemteka, akiwa hai na afya njema. Kamanda Mwabulambo alisema mtoto huyo alitekwa Sept

Mbunge Mteule Viti Maalum CUF, Bi Hindu Mwenda Azikwa

Image
Mwili wa marehemu Mbunge Mteule Viti Maalum Cuf, Hindu Mwenda, aliyefariki nyumbani kwake Kibada Kigamboni ukiwasili makaburi ya Kisutu Dar leo. Maziko yakiendelea. Sheikh (kulia) akifanya  maombi baada mazishi. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akiwa katika mazishi hayo. …Akiongea  na wanahabari baada ya maziko. HATIMAYE Mbunge Mteule Viti Maalum Cuf, Hindu Mwenda ,  aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni amezikwa leo makaburi ya Kisutu Dar na mamia ya wafuasi wa chama chake na wananchi wengine wa Dar es Salaam. Sheikh aliyeongoza mazishi hayo aliwahimiza wanachama wa Cuf kuendeleza upendo na kufanya kazi kwa ushirikiano ambapo miongoni mwao ni mwenyekiti wa chama hicho anayetembuliwa na Msajili wa Vyama, Profesa Ibrahim Lipumba. Lipumba alimsifia marehemu akisema alikuwa anajituma katika kazi zake na alikuwa mwanachama shupavu na alikuwa mfano kwa wanachama wengine wanaokipenda cha

Uhuru Kenyatta Ampa Onyo Raila Odinga

Image
Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta a mefunguka na kutoa onyo kwa mpinzani wake Raila Odinga kuwa asahu kuhusu tume mpya ya uchaguzi lakini pia amemtaka Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga kutoingilia kwani wao wameheshimu maamuzi ya mahakama. Uhuru Kenyatta mpinzani wake Raila Odinga (kushoto). Uhuru Kenyatta amesema chama chake cha Jubilee kipo tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na sasa wanasubiri Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC iweze kutangaza siku ya uchaguzi na wanaiomba itangaze siku hiyo haraka. Aidha Uhuru Kenyatta amesema kuwa wapinzani hao hawana haja ya uchaguzi bali ni watu ambao wanataka serikali ya mseto kitu ambacho yeye hawezi kukiruhusu hata kidogo Mahakama ya juu nchini Kenya Septemba 1, 2017 ilifuta matokeo ya Urais nchini Kenya na kuamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike katika nafasi ya Urais kutokana na mahakama hiyo kubaini baadhi ya mapungufu wakati wa utoaji wa matokeo hayo ya uchaguz

Waziri Mkuu Majaliwa atoa suluhisho la ajira

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani  vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana. Waziri Mkuu alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia. “Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa vijana kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake. Lakini mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija," Mhe. Majaliwa. Pamoja na hayo Majaliwa ameongeza na kusema kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko. Ha

Wema Sepetu atupa jiwe gizani

Image
 Malkia wa filamu Bongo , Wema Abraham Sepetu ametupa jiwe gizani ambalo bado halijajulikana ni kwenda kwa mtu gani na kumwambia bado wa kumshusha hajazaliwa kwani yeye alivyo ni majaaliwa kutoka kwa maulana na siyo kujitakia. Wema ametupa jiwe hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuna mtu kamuharibia siku hivyo na kumwambia kwamba yeye hakujitakia kuwa alivyo hivyo mtu huyo ajue kutofautisha. "Wa kunizima hajazaliwa bado jamani... Alafu mjue kutofautisha kati ya Kujaaliwa na kujitakia... Alhamdulillah nyingi kwa Maulana wangu... Sikujitakia... Ni majaaliwa tu... To whom it may Concern... Kuna mtu kajua kuniharibia siku wallah... " Wema Sepetu.  Dongo la Wema mtandaoni Aidha Wema ameongeza kwa kusema katu hawezi kujitutumua kwani anaogopa kujiumiza. Vilevile  tukio hilo linaunganishwa moja kwa moja na mtu ambaye Wema Sepetu amemuhisi anataka kujaribu kudukua mtandao wake wa Instagram hali iliyompelekea kumuandikia ujumbe kuwa katu hatam

UCHAGUZI KENYA: Mahakama Kuu imefuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa nchi hiyo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta. Imeamuru uchaguzi urudiwe ndani ya siku 60.

Image
  Mahaka Kuu ya Kenya. IDARA ya Mahakama imesema majaji wa Mahakama Kuu nchini Kenya wameanza kutoa uamuzi  kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyowasilishwa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (NASA) saa 5:00, leo ambapo ndiyo siku ya mwisho kikatiba kwa mahakama hiyo kutoa uamuzi. Matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi Kulikuwa na wagombea wanane katika uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti mwaka huu. Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa Ijumaa tarehe 12 Septemba na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: Ekuru Aukot 27,311 (0.18%) Abduba Dida 38,093 (0.25%) Cyrus Jirongo 11,705 (0.08%) Japheth Kaluyu 16,482 (0.11%) Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27%) Michael Wainaina 13,257 (0.09%) Joseph Nyagah 42,259 (0.28%) Raila Odinga 6,762,224 (44.74%) Waliokuwa wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ni 19,611,423 lakini waliopiga kura walikuwa 15,073,662 ambao ni sawa na asilimia 78.91. Ma

Rais Magufuli atoa samalu ya Eid kwa Waislam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa salamu kwa waumini wa dini ya Kiislam na kuwatakia sikuu njema ya Eid. Katika ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ametoa ujumbe huo kuwatakia Eid njema, huku akihimiza kudumisha amani, upendo na mshikamano. "Nawatakia Waislamu na watanzania wote sikukuu njema ya Eid el-Hajj, tunaposherehekea sikukuu hii tuendelee kudumisha upendo,amani,umoja na mshikamano wetu. Eid Mubarak", aliandika Rais Magufuli. Waumini wa dini ya Kiislam nchini leo wanaungana na Waislam wenzao wote duniani, kusherehekea sikuku ya Eid ambayo huadhimishwa kila mwaka, mara baada ya ibada ya Hija kukamilika, na mara nyingi husherehekiwa kwa kuchinja wanyama waliohalalishwa kwa binadamu.

Mahakama imeelezwa Sethi wa IPTL Amewekwa Puto Tumboni

Image
Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha. Mbali ya Seth, mwingine ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh 309,461,300,158. Wakili wa utetezi, Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama. ”Ugonjwa uliosababisha Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kuto

Hakimu Akataa Msokoto wa Bangi Kesi ya Wema

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imekataa kupokea ushahidi wa msokoto wa bangi na vipisi viwili vya madawa hayo ya kulevya katika kesi inayomkabili mwigizaji Wema Sepetu . Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Thomas Simba , aliyesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu.