Rais Magufuli atoa samalu ya Eid kwa Waislam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa salamu kwa waumini wa dini ya Kiislam na kuwatakia sikuu njema ya Eid.

Katika ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ametoa ujumbe huo kuwatakia Eid njema, huku akihimiza kudumisha amani, upendo na mshikamano.

"Nawatakia Waislamu na watanzania wote sikukuu njema ya Eid el-Hajj, tunaposherehekea sikukuu hii tuendelee kudumisha upendo,amani,umoja na mshikamano wetu. Eid Mubarak", aliandika Rais Magufuli.



Waumini wa dini ya Kiislam nchini leo wanaungana na Waislam wenzao wote duniani, kusherehekea sikuku ya Eid ambayo huadhimishwa kila mwaka, mara baada ya ibada ya Hija kukamilika, na mara nyingi husherehekiwa kwa kuchinja wanyama waliohalalishwa kwa binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA NA MWANAFUNZI WA UDOM ILI KUTANGAZA SOKO LA MWILI WAKE. TAZAMA HAPA

ZITTO KABWE AWAPONDA LOWASSA NA MAGUFULI