Posts

Muigizaji wa Siri za Familia apata ajali

Image
Luwi Cappelo Muigizaji wa filamu Luwi Cappelo wa nchini Kenya ambaye ameigiza tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na East Africa Television, amepata ajali ya gari na kulazwa hospitali ya Pandya mjini Mombasa Kenya, katika chumba cha wa wagonjwa Mahututi. Mkurugenzi wa Jasson Production ambao ndio watengenezaji wa tamthilia ya Siri za Familia, Bw. Sanctus Mtsimbe, amesema kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Lui akiwa njiani kuelekea Mombasa kwenye harusi huku akiwa na wenzake, lakini baadaye alipata taarifa za ajali hiyo. Hata hivyo Siri za Familia zimetoa taarifa rasmi ya ajali hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram, ukiandika...”Tumepata taarifa kupitia wenzetu wa Nairobi kuwa siku ya Jumapili saa 8 alfajiri, muigizaji wetu wa Siri za Familia msimu wa 4 kutoka Kenya Luwi na rafiki zake watatu, walipata ajali katika barabara ya Mombasa - Malindi wakiwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi. Luwi alikuwa amekaa nyuma na aliumia, kwa sasa Luwi amelazwa Hospita

HESLB Yaongeza Muda wa Uombaji Mikopo Vyuo Vikuu

Image
Mkurugenzi Mkuu wa HESLB, Abdul-Razaq Badru. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. “Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema. Amesema hadi kufikia jana Agosti 29 , wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.

VANESSA MDEE NA JUX ACHENI KUTUZUGA!

Image
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunizawadia pumzi yake ambayo imeniwezesha kuandika barua hii ya leo inayokufikia wewe msomaji ambaye pia umekuwa ukinisaidia kwa maoni na ushauri kuhusu safu yetu hii. Leo nina kazi ya kuzungumza na wanamuziki wawili ambao kwa muda mrefu, wametengeneza moja kati ya kapo bomba kabisa za wasanii wanaojihusisha kimapenzi. Unapozungumza kuhusu wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa katika Bongo Fleva, huwezi kuwaacha kando Jux na Vanessa ambaye ni maarufu kama Vee Money, kwani hivi sasa ni miongoni mwa vijana wanaotupa uwakilishi mzuri kimataifa, kwa sababu kazi zake ni moto barani Afrika. Binafsi ninawakubali, maana mimi pia ni muumini mkubwa wa aina ya muziki wanaofanya. Maisha ya kimapenzi ya wasanii hawa siku za nyuma, leo yamenisukuma niseme nao kidogo, hasa kwa kuangalia matukio yanayoendelea hivi sasa kati yao. Uhusiano wao uliingia dosari kwa namna ambayo hakuna hata shabiki mmoja alitegemea, maana ni kama kitu cha g

Majambazi wateka basi, wapora madiwani

Image
MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana. Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana. Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge. Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo. Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuk

Mawakili wamgomea Tundu Lissu

Image
MAWAKILI WA KUJITEGEMEA WAKITOKA MAHAKAMNI BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI ZAO KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM JANA. MAWAKILI wa kujitegemea wamekaidi kutii wito wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Mawakili (TLS) wa kutohudhuria mahakamani kwa siku mbili baada ya jana kujitokeza katika mahakama mbalimbali kutetea wateja wao. MAWAKILI wa kujitegemea wamekaidi kutii wito wa Baraza la Uongozi wa Chama cha Mawakili (TLS) wa kutohudhuria mahakamani kwa siku mbili baada ya jana kujitokeza katika mahakama mbalimbali kutetea wateja wao. Jumapili, baraza hilo kupitia Rais wa TLS, Tundu Lissu, lilitangaza maazimio matano likiwamo la kuwataka mawakili wote nchini kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza kwa siku mbili, jana na leo, ikiwa ishara ya kupinga kuvamiwa na kulipuliwa kwa bomu kwa ofisi ya kampuni ya uwakili ya IMMMA jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita. Mawakili jana walionekana kukaidi wito huo baada ya kuhudhuria ma

JOYCE KIRIA AELEZA BANGI ZILIVYOMKOMESHA

Image
  Joyce Kiria. MTANGAZAJI maarufu Bongo, Joyce Kiria amefunguka jinsi alivyokomolewa na kitendo chake cha kuvuta bangi, akidhani kingempa ujasiri, lakini badala yake akajikuta akishindwa kabisa kufanya kitu alichokusudia. Akizungumza na Za Motomoto News, Joyce alisema kwa mara ya kwanza alivuta bangi alipoanza utangazaji katika kituo kimoja cha redio kipindi hicho na alifanya hivyo ili apate ujasiri wa kutangaza kwani alikuwa hajui, lakini aliambulia kuona vitu viwiliviwili na kushindwa kabisa kutangaza. “Nimewahi kuvuta bangi mara moja ili niweze kutangaza maana nilikuwa naogopa, lakini nilipofika studio nikawa naona mic mbilimbili, watu wawiliwawili mwisho nikarudi nyumbani ambako nilikaa siku mbili nzima ndiyo nikawa sawa, sijawahi kurudia tena na sina mpango maana nilikoma siku hiyo,” alisema Joyce. STORI: GLADNESS MALLYA| RISASI

BREAKING NEWS: Lissu Awaongoza Mawakili Kugoma Kuingia Mahakamani

Image
Tundu Lissu akiakiwa na mawakili wengine wakati wakizungumza na wanahabari katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dar. RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda wa siku mbili Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita. “Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Dr. Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanahabari . Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi as

Mbunge wa Tunduma atakiwa kukamatwa

Image
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais. Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani ya Momba imeagiza kiongozi huyo kukamatwa baada ya kumdhihaki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Juma Said Irando.

Manara alalamikia Bodi ya ligi

Image
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kwa kuwatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa wanachokifanya siyo sawa wanabidi wabadilike. Manara ameeleza hayo baada ya Bodi hiyo kufanya mabadiliko ya ratiba za mechi zinazoshiriki katika Ligi Kuu ili kupisha mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Botswana iweze kuchezwa mnamo Septemba 2 mwishoni mwa juma hili. "Nimesikitika sana kuona kwamba ratiba ya Ligi Kuu imebadilishwa, mechi hizi zipo kwenye kalenda ya FIFA. Mnapanga ratiba mechi ya pili tu mnaanza kubadilisha ratiba kwa hiyo sisi mechi yetu na Azam FC haitakuwepo ?", alisema Manara Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "mnatupunguza ile nguvu tuliyoanza nayo, hili jambo nilishalisema sana kwa nini mnavyopanga ratiba zenu bodi ya Ligi msiwe mnaangalia kalenda ya FIFA. Hivi mshawahi kusikia wapi duniani mtu anabadilisha ratiba la

Tshirt na Jinsi ya Manji yazua gumzo

Image
Huku akitia huruma, baadhi ya wananchi jijini hapa wameibua gumzo kuhusiana na nguo anazovaa mfanyabiashara maarufu, Yusufu Manji ambaye ana kesi mbili zinazomkabili. Manji ambaye alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 17, mwaka huu amekuwa akikabiliwa na kesi mbili, moja ikihusu uhujumu uchumi na ya pili ni madai ya matumizi ya dawa za kulevya. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakidai kwamba wamekuwa wakimshuhudia Manji akija mahakamani akiwa amevaa tisheti ya rangi nyeusi kwa zaidi ya mara kumi, jambo ambalo limeleta gumzo kwa kuwa wanaamini ana nguo nyingi. “Hatujui sababu, huyu bwana ni tajiri sana lakini kila akifika mahakamani anavaa tisheti nyeusi ileile, kwa nini?” alihoji mwananchi mmoja. Wapo waliomuonea huruma na kudai kwamba inawezekana anafanyiwa figisufigisu kwa kutoruhusiwa kupelekewa nguo na wengine wanadai kwamba inawezekana ameamua mwenyewe awe hivyo kama alivyoamua kutonyoa ndevu. UWAZI liliamua kumtafuta mtaalamu wa utabiri (Astrologer

FAIDA ZA UGALI WA DONA

Image
MARA nyingi baadhi ya watu huwahimiza watu wengine kutumia unga wa mahindi au nafaka zingine usiokobolewa bila ya kubainisha hasara ya unga wa aina hiyo. Watu wengi (bila shaka hata wewe msomaji wa makala haya), hawako tayari kutumia unga usiokobolewa maarufu kama dona. Kuwalazimisha watu wa aina hiyo kutumia unga usikobolewa (unga wa dona) ni sawa na kuwaweka watu hao katika hatari ya kuwa na lishe duni. UNGA WA MAHINDI Unga wa mahindi, ulezi, uwele, mtama na kadhalika ni chanzo kikubwa kwa watu wengi barani Afrika cha virutubisho kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hata hivyo, namna ya usagaji na matumizi ya unga wa mahindi na nafaka hizo inaweza kuukosesha mwili faida ya virutubisho vilivyomo katika nafaka hiyo. UNGA ULIOKOBOLEWA Mahindi yaliyokobolewa yaani sembe au nafaka zingine zikikobolewa kama mtama, ulezi n.k hupoteza sehemu fulani ya nafaka hizo. Kama mahindi au mtama na ulezi utasagwa bila kukobolewa unga wake huitwa unga wa dona (whole-g

Zitto Kabwe: Rais Magufuli Akiniteua Nitakataa!

Image
Rais Magufuli (kulia) akisalimiana na Zitto Kabwe, kushoto ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa hatokubali endapo Rais Dkt Magufuli atamteua kushika nafasi yoyote ya uongozi kwani hatakuwa na fursa ya kukijenga chama chake ili kiwe tayari kushinda uchaguzi na kushika dola. Zitto ambaye chama anachotoka tayari kimetoa viongozi wawili ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira alisema endapo atateuliwa, atamshukuru Rais na kukataa uteuzi huo. Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi wakati akijibu swali kuhusu uteuzi wa viongozi wa chama chao ambao mmoja alikuwa mshauri wa chama na mwingine alikuwa mwenyekiti wa chama hicho kichanga Tanzania. “Sitakubali uteuzi kwa sababu jukumu langu na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo ni kujenga chama ili kupata ushawis

Msukuma amjibu tena Tundu Lisu

Image
Siku moja baada ya Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutoa wito kwa Mawakili wote ambao ni Wanachama wa chama hicho kususia shughuli za Mahakama, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amejitokeza na kumpinga. Licha ya kusikitishwa na kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa kwa Ofisi za IMMMA Advocates, Msukuma amesema kitendo cha Chama cha Mawakili kutangaza mgomo ni kutowatendea haki wateja wao kwa siku zote watakazoamua kususia shughuli za Mahakama. ”Watanzania kwa pamoja tunalaani kitendo kilichofanywa kwenye Ofisi za IMMMA Advocates kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kihalifu. Tunamuomba IGP Sirro afanye juu chini kuhakikisha watu hawa wanakamatwa. “Nilishtushwa sana na matamko yaliyotolewa na Rais wa TLS, Tundu Lissu jana kwamba anatangaza mgomo wa Wanasheria kuanzia kesho na keshokutwa. Najiuliza kama Tundu Lissu anatangaza mgomo wa Wanasheria, hiyo ndiyo hukumu ya kumpata mvamizi? “Nadhani Wanasheria waisaidie Polisi kumgundua ni nan

Jerry Muro Amtolea Povu la Mwaka Tundu Lissu

Image
Jerry Muro. ALIYEKUWA msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amemtolea povu Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu kutaka wanachama wote wa TLS kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili. Muro ameyaandika haya. Tundu Lissu, TUNDUNI  Na Jerry C. Muro  Nianze kwa kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA Advocates, bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS chama chenu ‘MAHIRI’ cha wanasheria Tanganyika – TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza rasmi safari ya kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusiana na tukio la IMMA Advocates. Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na “AKILI NDOGO” za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili. Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza

BREAKING: Polisi watoa taarifa Kuhusu tukio la mlipuko ofisi za mawakili

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 28/08/2017                TUKIO LA MLIPUKO KWENYE OFISI ZA MAWAKILI WA IMMA Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 26/8/2017 lilitoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam. Hivyo Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa  uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui. Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusaba

RAS-Dodoma- Wakumbukeni Idara za Elimu katika PlanRep Mpya.

Image
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dododma  Rehema Madenge akifungua mafunzo ya siku nane kwa wataalamu wa Afya, Mipango na Fedha kutoka Mikoa Mitano chini ya ufadhili wa mradi wa Uimarishaji Mifumo (PS3) Serikali mkoani hapa imesema ili mpango wa PlanRep uweze kufanikiwa kwa ufasaha hakuna budi kuzijumuisha idara za Elimu katika mafunzo yanayoendelea mkoani Dodoma yanayo wajumuisha wataalam wa mipango pamoja na afya kutoka mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na wenyeji Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya bajeti kwakutumia mfumo mpya wa PlanRep na FFARS. Akifungua mafunzo ya siku nane mkoani hapa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge, amesema moja ya vitu vilivyokuwa vikikwamisha masuala ya bajeti ni pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi huku akinyooshea kidole takwimu za idara za elimu. “Ninatamani sana takwimu za elimu ziwe sahihi hasa katika uwasilishaji wa taarifa za mitihani ili ziweze kuendana na idadi ya wanafunzi na fedha zinazo o

JAJI MKUU, POLISI WATOA ONYO MGOMO WA MAWAIKILI NCHI NZIMA

Image
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma. Kaimu  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam. Profesa Juma jana  alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake. Profesa Juma alisema uhuru wa mahakama ni pamoja na kuheshimu mamlaka nyingine za nchi zinapokuwa zinafanya kazi zake.  Alisema kwa kuwa tukio la kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa Immma ni tukio la kihalifu, hivyo wanasheria waiache Polisi na vyombo vingine vya upelelezi kufanya kazi yao. “Kama kutatokea wateja watakaolalamika kuwa mawakili wao hawakufika mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano, hatua

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA TAKUKURU

Image
Rais Maguduli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola (Picha na Maktaba). Ulinzi umeimarishwa katika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zilizoko Upanga, jijini Dar es Salaam huku ikielezwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatembelea ofisi hiyo. Saa 3:17  asubuhi yaleo  Agosti 28 , msafara wenye magari yapatayo 10 uliingia katika ofisi hiyo. Katika kuimarisha ulinzi, barabara zinazoingia kwenye ofisi hiyo nazo zimefungwa. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Rais alipotembelea TAKUKURU tutakujuza baadaye. Endelea kufuatilia habari zetu.

CHRISTINA SHUSHO AANDIKA UJUMBEE HUU KUHUSU WIMBO WA ALIKIBA SEDUCE ME

Image
Ni siku mbili sasa zimepita tangu mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ ambao umekuwa ukizungumziwa na watu mbalimbali wasanii na wasiokuwa wasanii na wanasiasa pia. Mmoja wa wasanii waliouzungumzia wimbo huo ni pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho ambaye anafahamika zaidi kutokana na nyimbo zake za kumsifu Mungu lakini kupitia Instagram yake aliandika huu ujumbe kwa Alikiba. ”Leo unaeza kuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha seduce me….eeh jamani Kiba we noma. – Wimbo ni mzuri sana Professionally in boss ruge ‘s voice. – Hauna picha za aibu , naeza watch na familia, though sijui maana ya SEDUCE ME. #team Kigoma #wamanyema oyeeeee LAST @OFFICIALALIKIBA BASI SIKU NYINGINE TUTEMBELEE KANISANI. UKIWA MFALME HUCHAGUI DINI WOTE WAKO.”

RC Makonda aamua kufunguka kuhusu Diamond na Alikiba

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dar ss Salaam Paul Makonda ameamua kuandika maoni yake kutokana na kile anachokiona kuhusu wasanii wa Bongofleva wanaoshindanishwa kimuziki ambao ni Alikiba na Diamond. RC Makonda ameaandika maneno 17 kwenye Instagram ambayo yanawahusu mastaa hao wanaotajwa kuwa wana ushindindani kimuziki akionesha kufuraishwa na kazi za mastaa hao lakini akiwaonya tofauti zao kutovuka mipaka na kuvunja sheria au tamaduni za kitanzania. “Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki. Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..” – RC Makonda