Manara alalamikia Bodi ya ligi


Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kwa kuwatupia lawama Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa wanachokifanya siyo sawa wanabidi wabadilike.

Manara ameeleza hayo baada ya Bodi hiyo kufanya mabadiliko ya ratiba za mechi zinazoshiriki katika Ligi Kuu ili kupisha mechi ya kirafiki baina ya Tanzania na Botswana iweze kuchezwa mnamo Septemba 2 mwishoni mwa juma hili.

"Nimesikitika sana kuona kwamba ratiba ya Ligi Kuu imebadilishwa, mechi hizi zipo kwenye kalenda ya FIFA. Mnapanga ratiba mechi ya pili tu mnaanza kubadilisha ratiba kwa hiyo sisi mechi yetu na Azam FC haitakuwepo ?", alisema Manara

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "mnatupunguza ile nguvu tuliyoanza nayo, hili jambo nilishalisema sana kwa nini mnavyopanga ratiba zenu bodi ya Ligi msiwe mnaangalia kalenda ya FIFA. Hivi mshawahi kusikia wapi duniani mtu anabadilisha ratiba la ligi katika mechi ya pili ? hii ni 'only' Tanzania, ingekuwa ya tisa au ya 10 hapo sawa lakini ya pili.

Kwa mengine mengi msikilize hapa chini Haji Manara akifunguka kuhusiana na kubadilishwa ratiba ya michuano na Bodi ya Ligi.

Comments

Popular posts from this blog