Msukuma amjibu tena Tundu Lisu


Siku moja baada ya Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutoa wito kwa Mawakili wote ambao ni Wanachama wa chama hicho kususia shughuli za Mahakama, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amejitokeza na kumpinga.

Licha ya kusikitishwa na kitendo cha kuvamiwa na kulipuliwa kwa Ofisi za IMMMA Advocates, Msukuma amesema kitendo cha Chama cha Mawakili kutangaza mgomo ni kutowatendea haki wateja wao kwa siku zote watakazoamua kususia shughuli za Mahakama.

”Watanzania kwa pamoja tunalaani kitendo kilichofanywa kwenye Ofisi za IMMMA Advocates kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kihalifu. Tunamuomba IGP Sirro afanye juu chini kuhakikisha watu hawa wanakamatwa.

“Nilishtushwa sana na matamko yaliyotolewa na Rais wa TLS, Tundu Lissu jana kwamba anatangaza mgomo wa Wanasheria kuanzia kesho na keshokutwa. Najiuliza kama Tundu Lissu anatangaza mgomo wa Wanasheria, hiyo ndiyo hukumu ya kumpata mvamizi?

“Nadhani Wanasheria waisaidie Polisi kumgundua ni nani. Kama kuna taarifa Tundu Lissu mpaka anafikia kusema tukigoma atapatikana aliyefanya haya matendo, aisaidie Polisi waweze kumkamata haraka.” – Joseph Msukuma.

Comments

Popular posts from this blog