Muigizaji wa Siri za Familia apata ajali

Luwi Cappelo
Muigizaji wa filamu Luwi Cappelo wa nchini Kenya ambaye ameigiza tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na East Africa Television, amepata ajali ya gari na kulazwa hospitali ya Pandya mjini Mombasa Kenya, katika chumba cha wa wagonjwa Mahututi.

Mkurugenzi wa Jasson Production ambao ndio watengenezaji wa tamthilia ya Siri za Familia, Bw.
Sanctus Mtsimbe, amesema kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Lui akiwa njiani kuelekea Mombasa kwenye harusi huku akiwa na wenzake, lakini baadaye alipata taarifa za ajali hiyo.

Hata hivyo Siri za Familia zimetoa taarifa rasmi ya ajali hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram, ukiandika...”Tumepata taarifa kupitia wenzetu wa Nairobi kuwa siku ya Jumapili saa 8 alfajiri, muigizaji wetu wa Siri za Familia msimu wa 4 kutoka Kenya Luwi na rafiki zake watatu, walipata ajali katika barabara ya Mombasa - Malindi wakiwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi. Luwi alikuwa amekaa nyuma na aliumia, kwa sasa Luwi amelazwa Hospitali ya Pandya. Tunaomba tumwombee Luwi apate kupona na kuendelea na shughuli zake za Maisha". ilisema taarifa hiyo.

Hali ya Luwi Cappelo bado si nzuri na bado anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Pandya, mjini Mombasa, lakini wenzake ambao alikuwa nao kwenye gari hawakupata majeraha makubwa.

Comments

Popular posts from this blog