RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA TAKUKURU



Rais Maguduli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola (Picha na Maktaba).
Ulinzi umeimarishwa katika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zilizoko Upanga, jijini Dar es Salaam huku ikielezwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatembelea ofisi hiyo.

Saa 3:17 asubuhi yaleo Agosti 28, msafara wenye magari yapatayo 10 uliingia katika ofisi hiyo.
Katika kuimarisha ulinzi, barabara zinazoingia kwenye ofisi hiyo nazo zimefungwa.
Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Rais alipotembelea TAKUKURU tutakujuza baadaye. Endelea kufuatilia habari zetu.

Comments

Popular posts from this blog