WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA:SERIKALI KULIPA MADENI YA WATUMISHI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali italipa madeni yote ya Watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali. Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliyofanyika kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora na Rais Pombe Magufuli alisitisha malipo kwa sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika na yale yaliyobainika kuwa halali yatalipwa huku akiwataka Watumishi hao wafanye kazi ya kuwadumia wananchi kwa bidii. "Hivi sasa tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi, hakuna madeni ya matibabu, ya likizo au ya masomo. Kila mtumishi anaruhusiwa kujiendeleza, lakini ni lazima kwanza aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuelezea nia yake na akikubaliwa, ndipo aanze kutuma maombi kwenye vyuo. Mtumishi akiamua kuomba chuoni moja kwa moja ndipo alete madai yale, hatapewa chochote kwa sababu ni nje ya utaratibu," alisema Ma