RC Makonda ametangaza Walemavu DSM kupewa miguu ya bandia bure
Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, akionyesha mfano wa miguu ya bandia leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanikiwa kupata miguu ya bandia itakayoweza kuwasaidia wananchi wenye mahitaji.
Miguu hiyo yenye thamani ya Shilingi Milion 800 itatolewa bila malipo
kwa wananchi waliopata ajali na kushimdwa kupata miguu hiyo kutokana na
kushindwa kumudu gharama za kununua miguu hiyo ambapo mguu mmoja
unagharimu Milion tatu.
Kwa mantiki hiyo amewatangazia wananchi wote wenye mahitaji ya miguu ya
bandia na hawana uwezo wa kumudu gharama kufika ofisini ya mkuu wa mkoa
siku ya Jumatatu na Jumanne kwaajili kukutana na wataalamu wa miguu
watakaochukua vipimo kwaajili ya kutengenezewa miguu kulingana na
maumbile yao.
Amesema miguu hiyo ya watu 200 itatolewa kwa awamu hii ya kwanza ambapo
kama mahitaji yatakuwa makubwa na wafadhili wakaongezeka itatolewa tena
kwa awamu nyingine lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kutotumia
magongo.
"Nimepewa kazi ya mkoa kuhudumia makundi yote, nafahamu kwenye mkoa
wangu wapo waliopata ajali na wengine wakavunjika miguu lakini pesa ya
kupata miguu ya bandia ili waachane na magongo kwao imekuwa ni moja ya
changamoto, kutokana na sababu hiyo nimeona vyema nifikiri namna ya
kuwasaidia wananchi ambao hawana uwezo ili waweze kupata, nimefanikiwa
kupata wadau watakaonipatia miguu ya kuhudumia wananchi 200" Alisema
Makonda.
Comments
Post a Comment