KIBITI: Wahalifu 13 wauawa na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka
kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13
katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo
la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti.
Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana
katika majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha makasha ya
risasi (magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa
yakitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni
Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa
Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni
Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus
Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13
ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya
vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika
eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya
Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki
2, pamoja na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha silaha aina
ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na
wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la
Polisi katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi,
Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP)
Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la
Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi
La Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa
Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka
kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya
risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu. – Picha
na Jeshi La Polisi
Comments
Post a Comment