SAIDA KAROLI ASIMULIA JINSI ALIVYOIBIWA KAZI ZAKE KISA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA
Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo .Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea. ”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja ...