MTANGAZAJI DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM LEO

Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka.Kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani.Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile walichokuwa wanafanya.
Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town.Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Kwefeee ukipenda Fetty siku ya kesho anadondoka mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja Xxl kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mjengoni kupiga show along side Mammi Babbie pamoja na Dj Sinyorita! Kukamilisha mzunguko kamili wa #MalkiaWaNguvuDj Fetty ni baadhi ya Madj wakike wachache walioweka hamasa kwenye game ya bongo Fleva na kutoa nafasi ya kuzaliwa Madj wengine wakike kufuata nyanyo kwenye Udj!
Kesho inapofika Saba kamili mchana Tune ua Favourite Station Clouds Fm kuisikia sauti ya Dj Fetty.
Dj fetty kesho anarejea mjengoni kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani na kuonyesha kizazi kipya ubunifu wa Enzi zake je sauti ile ipo ama ishapotea.

Comments

Popular posts from this blog