Paul Makonda Aenda Mapumziko ya Miezi Miwili South Africa

Wakati utata ikigubika kuhusu safari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa kiongozi huyo atakuwa likizo nchini humo kwa zaidi ya miezi miwili.
Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa katika gazeti la TanzaniaDaima imeeleza uwepo wa RC Makonda nchini Afrika Kusini ndio sababu ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo ilitangazwa kuwa angekuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Mwembeyanga.
Kuondoka kwake nchini kumekuwa kwa kutatanisha wakati mamlaka husika zikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusuana na safari yake. Wadadisi wa mambo wanahoji uhalali wa Makonda kupewa mapumziko hayo nje ya nchi huku serikali ilitangaza kuzuia ziara zote za watumishi nje ya nchi ili kubana matumizi.
Kutokana na zuio la safari za nje ya nchi kwa watumishi wa umma lililotolewa na serikali ya awamu ya tano, safari hiyo ya Paul Makonda imeibua utata juu ya uhalali wake huku mamlaka husika zikirushiana mpira juu ya nani wakuzungumzia safari ya kiongozi huyo.
Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas alipoulizwa kama safari ya Makonda nje ya nchi yupo kikazi au binafsi alisema kuwa, swali hilo aulizwe Katibu Tawala wa Mkoa kwani ndiye mtendaji wake. Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando alipoulizwa alisema kuwa, swali hilo atafutwe Makonda mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog