WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA
Jeshi
la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za
kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo
sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita
dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za
Mvomero, Morogoro manispaa na Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa
wakisafirisha dawa hizo kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko
Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na
pikipiki maarufu kama boda boda.
Baadhi ya
watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana na dawa hizo, wamekuwa na majibu
tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na
bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi
mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo akidai alitumwa na mtu
bila kujua mzigo huo kama ni bangi, ambapo polisi wameomba ushirikiano
zaidi kuwabaini na kufichua matukio ya dawa za kulevya na watuhumiwa
wake.
Comments
Post a Comment