SAIDA KAROLI ASIMULIA JINSI ALIVYOIBIWA KAZI ZAKE KISA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA
Jana
kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi
alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa
hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na
Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai
zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye
haki nazo
.Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao
Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure
kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.
”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja

“Meneja
wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe idhini
yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya kuwa sauti
yangu imesikika kule, mimi nilimjibu nimeshakata tamaa na kuimba naona
muziki kwangu hauna faida na thamani bora kuwa hata mkaanga vitumbua au
maandazi kuliko kuimba”Nilikuwa na mpango wa kurudi kijijini nyumbani
nikae mtu akihitaji show atanikuta kijijini lakini meneja akanambia
hapana, alisema nyimbo tumpe Diamond kwa sababu itaniinua na kunipa moyo
na kuniamsha upya kama mtu aliyekufa“Walizushaga nimekufa na nilihisigi
nimekufa kweli kutokana na hali ya maisha na nilikuwa nimekata tamaa
nikajua nimekufa kweli” AlisemaSaida KaroliKwa sasa Saida yupo Dar na
amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki upya kama zamani na yupo
tayari kufanya kolabo na wasanii kama Ben pol, Bell 9, Diamond na
Darassa.
Comments
Post a Comment