Mama Mlezi wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afariki Dunia
Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika
Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo.
Kupitia mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru
jamii kwa salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko
nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko
yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri.
“Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu,
Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998.
Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee
Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo”. Kauli
ya Jakaya Kikwete
Naye Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa
marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho
asubuhi ya leo.
“Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi
yetu Bi. Nuru Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali
ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi
tutajulishana” Amesema Ridhiwan Kikwete.
Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo
kufuatia kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi.
– JK— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. – JK
Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo. – JK
Mama yetu mdogo aliitwa jana na Mola, na kuitika. Shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo. – JK
Mazishi yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri. – JK
Comments
Post a Comment