Posts

Uwoya ni Gusa Unate!

Image
DAR ES SALAAM: Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani)  anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kuachwa. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Uwoya aliyeomba hifadhi ya jila lake, staa huyo mwenye shepu na mvuto wa kudatisha kimahaba amekuwa akipapatikiwa sana na wan aume lakini mwisho wa siku huishia kuwaliza kwani yeye ndiye anayeamua kuendelea na wewe au akuache. “Uwoya namjua vizuri sana, yule ni hatari kwa wanaume. Kwanza anajijua kuwa ni mzuri hivyo amekuwa akiwadenguliwa wanaume wengi sana na orodha ya wanaomtokea kila siku ni kubwa. “Lakini akitokea kukupenda atakupenda kweli hadi unaweza kuona kero. Kwa kifupi anajua kupenda, kujali na kubembeleza kiasi kwamba ukinasa kwake ni vigumu kutoka ndiyo maana wapo wanaosema kwamba, Uwoya ni gusa unate! “Ila sasa, anaweza kukuchanganya kwa mahaba mazito lakini siku akiamua kukuacha, a...

BREAKING NEWZZ:MMILIKI WA HANDAKI LA CD ZA UJANJA UJANJA ATIWA MBARONI NA POLISI

Image
Mmiliki wa hoteli ya Butterfly iliyopo maeneo ya Kariakoo, Phili Ulaya Mdolo maarufu kwa jina la Dotto ametiwa mbaroni kutokana na tuhuma za kumiliki duka kubwa la CD lililopo mafichoni ndani ya hoteli yake hiyo bila kufuata utaratibu wa serikali. Dotto amekamatwa Ijumaa hii katika operesheni iliyoongozwa na Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ya kukagua maduka yanayouza CD kinyume na sheria pamoja na maeneo yanayozalisha CD feki. Waziri Nape amesema kuwa huyo ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa jijini Dar es Salaam ambao wanafanya biashara hiyo bila kufuata taratibu za serikali huku akiliamuru jeshi la polisi kumshikilia mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi huku akiahidi kukutana naye siku ya Jumatatu. Tazama picha zaidi hapa chini za tukio hilo. Waziri Nape akiongoza kukagua baadhi ya vyumba vilivyopo chini ya ardhi katika hoteli ya Butterfly Kufuli ikivunjwa katika sehemu zilizohifadhiwa CD haramu katika hotel...

PICHA: WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KARIAKOO, AKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII

Image
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye leo ameongoza timu yake katika operesheni maalumu ya kufanya msako mkali wa wauzaji wa kazi za wasanii bila vibali vya Bodi ya filamu ya Tanzania.  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia bidhaa za filamu na muziki zilizofeki leo hii. Waziri huyo amevamia maduka yanayouza CD FEKI pamoja na ofisi ambayo inajihusisha na kurudufu kazi za wasanii kutoka ndani na nje ya nchini. Hii ni ziara ya Pili kuifanya Kariakoo. Ziara ya kwanza ya kushitukiza aliifanya July 15, 2016 ambapo aliwataka wauzaji wa CD kote nchini kufuata sheria ya kuuza CD zenye stika huku akisema mtu yoyote ambaye atakutwa na CD ambayo haina stika mnunuaji na muuzaji wote watakamatwa. Operesheni hizi zinafanywa kwa lengo la kutokomeza uharamia wa bidhaa za filamu na muziki kwa kuokoa pato la TAIFA Amesema Seikali itawachukulia hatua za kisheria ikiweemo kuwafutia leseni wauzaji na wasambazaj...

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga  Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre...

KAMANDA MPINGA AONGELEA WITO WA DIAMOND PLATNUMZ KITUO CHA POLISI

Image
Moja kati ya vitu ambavyo vilimake headlines kinoma noma siku ya jana ni pamoja na hii ya picha iliyosambaa ikimuonyesha msanii wa Bongo Fleva  Diamond Platnumz  akiwa kituo cha Polisi akifanyiwa mahojiano. Kitu ambacho kilizua maswali mengi sana kwa watu na wengine kuhisi kwamba huenda ni lile sakata la madawa ya kulevya linaloendelea kutikisa jiji la Dar es Salaam. Perfect255  ikaona isiwe kesi, ikapiga story na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani  Kamanda Mpinga  ili atusanue kuhusu mkanda mzima uliokuwa ukiendelea hapo jana kituo cha Polisi. “Ni kweli nilikuwa nimemwita Diamond aripoti hapa kwangu toka Jumanne, baada ya kuiona ile clip ambayo ilikuwa imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambayo ilifanana na yule kijana ambaye alikuwa akiimba wimbo wa Darassa, tukaona kuna haja ya sisi kuchukua hatua kwasababu tuliona jinsi alivyokuwa akiendesha alikuwa anavunja sheria za usalama barabarani.”

MBUNGE RIDHIWAN KIKWETE AFUNGUKA KUHUSU UTAJILI WAKE

Image
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya watu kuwa ana utajiri wa kutisha na kwamba anamiliki mali nyingi, jambo ambalo limekuwa likifanya watu hao watilie shaka njia aliyotumia kupata utajiri huo. Kikwete akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast ndani ya EA radio, amesema kuwa anashangazwa na dhana hiyo potofu inayojengwa na watu bila kujua ukweli wa mambo, ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni kijana mpiganaji na mwenye kupenda mafanikio, lakini hana umiliki wa mali nyingi kama ambavyo imekuwa ikisemwa. Ridhiwan ambaye ni mtotot wa Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amesema mali zake ni za kawaida na amezipata kwa njia halali, huku akisimulia jinsi alivyowahi kuwakuta watu wakimjadili yeye kuhusu mali zake, bila watu hao kujua kuwa yeye ndiye Ridhiwan Kikwete.

MAJALIWA ATETA NA MBUNGE WA SIMANJIRO

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia kwaya ya Wamasai wa Simanjiro wakati alipowasili kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjairo mjini Orkesimet Februari 16, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zana za asili za kabila la wamasai wakati aliposimikwa kuwa Mzee wa Simanjiro na kupewa jina la Ole Majaliwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mji Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mjini Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA DAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO

Image
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukubi wa Mwalimu Nyerere JNCC Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa.Rc Makond amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkuu w...

BREAKING NEWZ TID AOMBA RADHI KWA KUTUMIA ‘UNGA’, AWAPA NENO WANAOHOFIA ATAWATAJA

Image
Khaled Mohammed, maarufu kama Top In Dar es Salaam (TID), kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya na kuwaomba radhi watanzania kwa ujumla. Akizungumza muda mfupi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya awamu ya tatu ya wanaotuhumiwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, TID amesema kuwa ameamua kuachana na dawa za kulevya na kwamba sasa anaunga mkono vita dhidi ya dawa hizo. “Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji na mwenye nguvu mpya. Lakini niko hapa mbele yenu kama mnyama, narudia tena mnyama… na niko tayari kuungana na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,” amesema. “Unapaswa kuwa mnyama kama kaka yangu Makonda ili uweze kuishinda,” ameongeza. Ameongeza kuwa hakuna anayefahamu amepitia mangapi hadi kufikia hapo alipo leo na uamuzi wa kuacha dawa za kulevya akidai kuwa huenda ilihitajika nguvu ya dola kumsukuma...

Kajala Afunguka Kutomuona Wema Sepetu Selo

Image
Baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu kusota lupango kwa siku kadhaa kufuatia kutajwa kwenye tuhuma za madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kabla ya kupandishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, staa mwenzake, Kajala Masanja ameibuka na kufunguka sababu ya kutokwenda kumuona mahabusu. Kajala, akiwa ni rafiki wa Wema, aliwahi kuokolewa kwenda jela na mrembo huyo baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13, anadaiwa kutofika lupango katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’ jijini Dar alikokuwa ameshikiliwa Wema, jambo ambalo liliwashangaza wengi. Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, kitendo cha kutokwenda kumuona wala kufika mahakamani siku aliyopandishwa kizimbani, kilimuumiza Wema na ndugu zake kwani hawakutegemea mtu kama Kajala angeshindwa kufika kumuona na kumsapoti shosti wake huyo. Katika mitandao ya kijamii, gumzo lilikuwa ni Kajala kutokwenda selo kumuona Wema hadi akatoka huku watu ...

HAWA NDIO WALIOTIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO

Image
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro . Akitangaza majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa ...

RAIS JOHN MAGUFULI LEO AMEMTEUA ROGERS W. SIANGA KUWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Image

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.  Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage. Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto), Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughul...

UPDATES: IDD AZZAN AWASILI KITUO CHA POLISI CHA KATI KWA AJILI YA MAHOJIANO

Image
Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo cha polisi cha kati kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa. Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam. Jana. Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema ifikikapo saa 7 mchana atazungumza na waandishi wa habari.