MBUNGE RIDHIWAN KIKWETE AFUNGUKA KUHUSU UTAJILI WAKE
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amefunguka kuhusu madai ya
baadhi ya watu kuwa ana utajiri wa kutisha na kwamba anamiliki mali
nyingi, jambo ambalo limekuwa likifanya watu hao watilie shaka njia
aliyotumia kupata utajiri huo.
Kikwete
akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast ndani ya EA radio,
amesema kuwa anashangazwa na dhana hiyo potofu inayojengwa na watu bila
kujua ukweli wa mambo, ambapo ameweka wazi kuwa yeye ni kijana mpiganaji
na mwenye kupenda mafanikio, lakini hana umiliki wa mali nyingi kama
ambavyo imekuwa ikisemwa.
Ridhiwan
ambaye ni mtotot wa Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete,
amesema mali zake ni za kawaida na amezipata kwa njia halali, huku
akisimulia jinsi alivyowahi kuwakuta watu wakimjadili yeye kuhusu mali
zake, bila watu hao kujua kuwa yeye ndiye Ridhiwan Kikwete.
Comments
Post a Comment