Kajala Afunguka Kutomuona Wema Sepetu Selo


Baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu kusota lupango kwa siku kadhaa kufuatia kutajwa kwenye tuhuma za madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kabla ya kupandishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, staa mwenzake, Kajala Masanja ameibuka na kufunguka sababu ya kutokwenda kumuona mahabusu.
Kajala, akiwa ni rafiki wa Wema, aliwahi kuokolewa kwenda jela na mrembo huyo baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13, anadaiwa kutofika lupango katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’ jijini Dar alikokuwa ameshikiliwa Wema, jambo ambalo liliwashangaza wengi. Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, kitendo cha kutokwenda kumuona wala kufika mahakamani siku aliyopandishwa kizimbani, kilimuumiza Wema na ndugu zake kwani hawakutegemea mtu kama Kajala angeshindwa kufika kumuona na kumsapoti shosti wake huyo.
Katika mitandao ya kijamii, gumzo lilikuwa ni Kajala kutokwenda selo kumuona Wema hadi akatoka huku watu wengine wakimporomoshea matusi.
Katika kuujua ukweli na sababu za kutokwenda kumuona rafiki yake huyo, Wikienda lilimtafuta Kajala ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nimeshazoea kutukanwa bila sababu lakini mimi sikuwepo, nilisafiri ndiyo maana sikwenda na nimeumia sana kutokwenda.”
Wema ni miongoni mwa mastaa na watu mbalimbali waliotajwa hivi karibuni na Makonda wakituhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo Jumatano iliyopita alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na dada wawili wa kazi ambapo walitoka kwa dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja.

Comments

Popular posts from this blog