BREAKING NEWZZ:MMILIKI WA HANDAKI LA CD ZA UJANJA UJANJA ATIWA MBARONI NA POLISI
Mmiliki wa hoteli ya Butterfly
iliyopo maeneo ya Kariakoo, Phili Ulaya Mdolo maarufu kwa jina la Dotto
ametiwa mbaroni kutokana na tuhuma za kumiliki duka kubwa la CD
lililopo mafichoni ndani ya hoteli yake hiyo bila kufuata utaratibu wa
serikali.
Dotto amekamatwa Ijumaa hii
katika operesheni iliyoongozwa na Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na
Michezo, Nape Nnauye ya kukagua maduka yanayouza CD kinyume na sheria
pamoja na maeneo yanayozalisha CD feki.
Waziri Nape amesema kuwa huyo
ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa jijini Dar es Salaam ambao
wanafanya biashara hiyo bila kufuata taratibu za serikali huku
akiliamuru jeshi la polisi kumshikilia mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kutoa
maelezo zaidi huku akiahidi kukutana naye siku ya Jumatatu. Tazama
picha zaidi hapa chini za tukio hilo.
Waziri Nape akiongoza kukagua baadhi ya vyumba vilivyopo chini ya ardhi katika hoteli ya Butterfly
Kufuli ikivunjwa katika sehemu zilizohifadhiwa CD haramu katika hoteli ya Butterfly
Mizigo ya CD ikiwa stoo katika hoteli ya Butterfly
Comments
Post a Comment