HAWA NDIO WALIOTIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad
Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na
usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
JESHI la
Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa
kuhusika katika kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku
likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na
kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa.
Kukamatwa
kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako
mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro .
Akitangaza
majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro
,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema
watuhumiwa hao tayari wamekamatwa na wako katika hatua mbalimbali za
kiupelelezi na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani.
Miongoni
mwa watuhumiwa 47 wamo watoto wawili waumri wa miaka 17 ambao ni
Wilfred Mnubi mkazi wa Bomang’ombe wilaya ya Hai na Ruben Bakari mkazi
wa Njoro katika manispaa ya Moshi.
Kati ya watuhumiwa hao wanawake ni 15 na wanaume ni 32 akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 60,Christina Ferdinand.
“Vita hii
tumeianza tangu mwaka juzi,tunajua vita hii ni kubwa bahati nzuri ni
kwamba njia wanazotumia wafanyabiashara wa dawa za kulevya husani
mirungi na bhangi ,tayari jeshi la polisi limezibaini,maeneo ambayo dawa
za kulevya zimekithiri Jeshi la polisi limekwisha baini ,operesheni hii
ambayo tumeianza ni endelevu na tutaendelea kuwakamata watu hawa kwa
kutumia mbinu zote tulizonazo.”alisema Mutafungwa
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza juu ya
msako mkali ulioanza wa kuwakamata wafanyabiashara wa dawa za kulevya
katika mkoa wa Kilimanjaro.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akinyunyiza marashi
juu ya Mirungi iliyofungwa katika vipande vya magazeti ikiwa ni mbinu
mpya inayotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa hizo.
Waliotajwa na kushikiliwa na jeshi la Polisi ni pamoja na:
(1) Juma Kabwele(25).
(2) Mohaed Kabwele (29) .
(3) Shabani Mponda(39).
(4) Khadija Mushiri(27).
(5) Veronika Chuwa (39).
(6) Mwanahamis Hussein.
(7) Yusuph Issa(42).
(8) Salim Massawe(48).
(9) Hadija Mohamed(50).
(10) Shenein Abilah(41).
(11) Husna Mgonja(24).
(12) Najima Desouza (46) .
(13) Ruben Bakari (17) .
(14) Paul Kisoka (26).
(15) Raphael Mbuya (40).
(16) Wilfred Mnubi(17).
(17) Athuman Swaehe (35).
(18) Joseph Hamis(20).
(19) Zuber Temu(27).
(20) Robert Kitika (18) .
(21) Mohamed Juma (25).
(22) Ahmad Shaban (57).
(23) Donas Masashua(22).
(24) Japhet Tungai (46).
(25) Asima Mndeme (24).
(26) Muutaz Zalia ,
(27) Noah Singano (29).
(28) Ramadhan Masale (40) .
(29) Kirambati Swai(45).
(30) Said Mrii.
(31) Erick Henry (20).
(32) Seif Ally(20).
(33) Ramadhan Hassan (36).
(34) Victor John(22).
(35) Upendo Endkia (42).
(36) Asia Ally(39).
(37) Catherine Linusi (36) .
(38) Mariam Hemed (44) .
(39) Mwajuma Msuya (48).
(40) Juma Yusuph (22) .
(41) Hussein Anyokisye (17).
(42) Musa Msangi (30).
(43) Ramadhani Hassan (36).
(44) Wilfred Munubi(17)
(45) Ruben Bakar.(17)
(46) Christina Ferdinand.(60)
(47) Samweli Kingai(42).
Comments
Post a Comment