PICHA: WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KARIAKOO, AKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye leo ameongoza
timu yake katika operesheni maalumu ya kufanya msako mkali wa wauzaji wa
kazi za wasanii bila vibali vya Bodi ya filamu ya Tanzania.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia bidhaa za filamu na muziki zilizofeki leo hii.
Waziri
huyo amevamia maduka yanayouza CD FEKI pamoja na ofisi ambayo
inajihusisha na kurudufu kazi za wasanii kutoka ndani na nje ya nchini.
Hii
ni ziara ya Pili kuifanya Kariakoo. Ziara ya kwanza ya kushitukiza
aliifanya July 15, 2016 ambapo aliwataka wauzaji wa CD kote nchini
kufuata sheria ya kuuza CD zenye stika huku akisema mtu yoyote ambaye
atakutwa na CD ambayo haina stika mnunuaji na muuzaji wote watakamatwa.
Operesheni hizi zinafanywa kwa lengo la kutokomeza uharamia wa bidhaa za
filamu na muziki kwa kuokoa pato la TAIFA
Amesema
Seikali itawachukulia hatua za kisheria ikiweemo kuwafutia leseni
wauzaji na wasambazaji wa filamu nchini ambao wamekuwa wakiuza bidhaa
hizo bila vibali kutoka kutoka mamlaka husika jambo ambalo likiikosesha
serikali mapato pamoja na kuchangia momonyoko wa maadili katika jamii.
Comments
Post a Comment