KAMANDA MPINGA AONGELEA WITO WA DIAMOND PLATNUMZ KITUO CHA POLISI
Moja
kati ya vitu ambavyo vilimake headlines kinoma noma siku ya jana ni
pamoja na hii ya picha iliyosambaa ikimuonyesha msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz akiwa kituo cha Polisi akifanyiwa mahojiano.
Kitu
ambacho kilizua maswali mengi sana kwa watu na wengine kuhisi kwamba
huenda ni lile sakata la madawa ya kulevya linaloendelea kutikisa jiji
la Dar es Salaam.
Perfect255 ikaona isiwe kesi, ikapiga story na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mpinga ili atusanue kuhusu mkanda mzima uliokuwa ukiendelea hapo jana kituo cha Polisi.
“Ni
kweli nilikuwa nimemwita Diamond aripoti hapa kwangu toka Jumanne,
baada ya kuiona ile clip ambayo ilikuwa imesambaa kwenye mitandao ya
kijamii, ambayo ilifanana na yule kijana ambaye alikuwa akiimba wimbo wa
Darassa, tukaona kuna haja ya sisi kuchukua hatua kwasababu tuliona
jinsi alivyokuwa akiendesha alikuwa anavunja sheria za usalama
barabarani.”
Comments
Post a Comment