WAJIUA HUKU WAKIJIREKODI FACEBOOK
Jay Bowdy (Kushoto) na Nakia Venant (Kulia). MWANAUME mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Jay Bowdy, 34, ambaye pia ni muigizaji chipukizi amekutwa akiwa amejiua garini huku taarifa zikisema kwamba kabla ya kujiua, aliwaambia wafuasi wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook kwamba anajiua hivyo wawapigie simu polisi kutoka hapo Los Angeles na kuwaambia kwamba alikuwa akijiua. Baada ya kupewa taarifa na raia wema, polisi kutoka katika kituo kikuu hapo Los Angeles walijaribu kumpigia jamaa aliyelipaki gari lake katika ya Mitaa ya Cumpston na Fulcher lakini hawakuweza kumpata kwa kuwa tayari alikuwa amekwishatekeleza kile alichokitaka. Watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo katika video hiyo iliyokuwa ikirekodiwa ‘live’ walipigwa na bumbuwazi kwani wengi walihisi kwamba alikuwa akiigiza kutokana na kazi yake hiyo kumbe mshikaji alikuwa akijiua kweli. Baadaye video hiyo ikatolewa mtandaoni na Facebook. SABABU YA KUJIUA Chanzo kilichokuwa ha