BREAKING NEWS : RAIS WA MAREKANI TRUMP AFUTA UFADHILI KWA MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA
Donald Trump amerejesha utekelezwaji wa Sera ya Jiji la Mexico
Rais wa
Marekani Donald Trump ametia saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku
kutolewa kwa pesa za serikali ya Marekani kufadhili mashirika ya nchi za
nje ambayo yanatekeleza au kutoa habari kuhusu utoaji mimba.Afisa wake
wa mawasiliano Sean Spicer amesema hatua hiyo ya rais inaonesha kwamba
"anataka kuwatetea Wamarekani wote, wakiwemo wale ambao hawajazaliwa."
Agizo
hilo ambalo kirasmi linafahamika kama "the Mexico City Policy" (Sera ya
Jiji la Mexico) huenda likayakera makundi ya kutetea uhuru wa wanawake
kuamua kuhusu uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na msimamo wake wa
kupinga utoaji mimba.Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba upigwe marufuku
Marekani.Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku dhidi ya ufadhili wa
mashirika ya utoaji mimba nje ya Marekani kutolewa.Rais wa Republican
Ronald Reagan mara ya kwanza alianzisha Sera ya Jiji la Mexico mwaka
1984 na kuwa wa kwanza kupiga marufuku ufadhili huo.
Lakini chama cha Democratic kilibatilisha marufuku hiyo chini ya utawala wa Bill Clinton.
Sera hiyo
inayataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanapokea ufadhili wa
serikali ya Marekani kukubali "kutotekeleza na kutoendeleza au
kutohamasisha watu watumie utoaji mimba kama njia ya uzazi wa mpango
katika nchi nyingine".Kwa miongo mingi, imekuwa kwamba pesa za Marekani
haziwezi kutumiwa katika utoaji mimba katika mataifa ya nje.
Lakini Sera ya Jiji la Mexico inaenda hatua zaidi.
Mwaka
2009, Barack Obama alisitisha utekelezaji wa sera hiyo, ambayo ilikuwa
imrejeshwa chini ya utawala wa Rais George Bush.Makundi ya kutetea uhuru
wa wanawake kuamua kuhusu uzazi wamepinga hatua hiyo ya Bw Trump."Ni
jambo la kusikitisha sana kwamba moja ya hatua za kwanza za Trump
inaunganisha mambo mawili kwa pamoja: kunyamazisha wote wanaotofautiana
naye na kuwakandamiza wanawake," taarifa kutoka kwa kundi la Naral
Pro-Choice America imesema.
"Siku
mbili baada ya maandamano ya kihistoria ya wanawake ya kumpinga Trump
kufanyika na siku moja baada ya maadhimisho ya uamuzi wa kihistoria wa
mahakama kesi ya Roe v. Wade, Donald Trump anapatia kipaumbele hatua ya
kurejesha ... sera ambayo inawanyamazisha wahudumu wa afya na kuweka
hatarini wagonjwa."Wakati wa kampeni, Bw Donald Trump, ambaye awali
alitetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu uzazi, aliambia MSNBC kwamba
"lazima kuwe na aina fulani ya adhabu kwa mwanamke" iwapo utoaji mimba
utakuwa marufuku.Baadaye, aliondoa tamko hilo baada ya kushutumiwa
vikali na makundi ya kutetea haki za wanawake.Agizo hilo limetolewa siku mbili baada ya wanawake kuandamana Washington na miji mingine kumpinga Trump
Maafisa
wa kampeni wa Bw Trump walisema waliamini uamuzi kuhusu uhalali wa
utoaji mimba unafaa kuachiwa majimbo yenyewe, na kwamba adhabu inafaa
kutolewa kwa wanaotoa huduma za utoaji mimba.Alisema anaunga mkono
marufuku ya utoaji mimba ila tu wakati mimba imetokana na "ubakaji,
kujamiiana kwa maharimu au wakati maisha ya mama yamo hatarini".
Bw Trump
pia ameahidi kujaza nafasi ya jaji iliyo wazi Mahakama ya Juu na jaji
ambaye ni mhafidhina kuhusu masuala ya kijamii.Hayo yakijiri, Bunge la
Congress limeashiria nia yake ya kuondoa ufadhili wa serikali kwa kundi
la Planned Parenthood, kundi linalotoa huduma za afya ya uzazi Marekani
na nje ya taifa hilo.
Comments
Post a Comment