JAJI CHANDE: NAFURAHI KUUACHA MUHIMILI WA MAHAKAMA KATIKA HALI NZURI
Jaji
Mkuu Mstaafu Mohamedi Othman Chande amezitaka mahakama kufanya kazi kwa
kuendana na kasi ya awamu ya tano pamoja na kufuata maadili ya taaluma
ya sheria katika kutoa haki na sawa kwa wakati na kwa watanzania wote.
Jaji Mkuu Mstaafu - Mohamed Chande Othman
Jaji
Chande ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma ambapo amesema kuwa kuongezeka kwa
uwazi katika shughuli za mahakama kutasaidia sana katika kuendeshwa kwa
kesi na kuamuliwa kwa wakati na watendaji wake.
Amesema
anafurahi anauacha muhimili wa mahakama katika hali nzuri huku akiwataka
watendaji kuendeleza juhudi za kuboresha mifumo taratibu na sheria ili
kutoa nafasi zaidi kwa kesi nyingi kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo
usikilizwaji wa kesi.
Akizungumzia
kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao ameuacha amesema
kuendelezwa kwa mpango huo kutasaidia kuharakisha usikilizaji wa kesi,
kuongeza mfumo wa usikilizwaji wa kesi pamoja na ushirikiano na ofisi ya
mwanasheria mkuu, mkurugenzi wa mashikata pamoja na polisi ikiwemo
uboreshaji wa njia ya kuwahudumia wateja wengi zaidi.
Rais Magufuli na majaji wa Mahakama ya Rufaa mara baada ya kumuapisha Kaimu Jaji Mkuu
Akieleza
kwa upande wa mahakama ya mafisadi amesema kuwa mahakama hiyo ni ya juu
na kuwa suala la rushwa na ufisadi zinashughulikiwa katika ngazi hiyo
licha ya kuwepo kwa utaratibu wa kusikilizwa kwa kesi ambazo tayari
zimekamilika kwa upande wa upelelezi pamoja na ushahidi ili kurahisisha
kumaliza kesi kwa wakati.
“Tumepokea
maombi matatu ambayo ni ya dhamana lakini nadhani mwaka huu hasa kesi
zinaweza zikaanza katika kanda 13 za mahakama kuu” alisema Jaji Chande
Rais Magufuli akimuapisha Kaimu Jaji Mkuu
Comments
Post a Comment