MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE
Na Woinde Shizza,Arusha
Mfanya
biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa
Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya
kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na
baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.
Mbele ya
hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka
wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11
mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa
yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia
mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .
Mwendesha
mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia
mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha
polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani.
Baada ya
kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe
alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa
jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo. Katika
shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri
unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati
ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo
imepangwa kusikilizwa february 6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.
Aidha
katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph
anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo
waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro
ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho. Alisema ameishi na
mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara
kadhaa bila mafanikio,
Comments
Post a Comment