MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHAI CHA LUPEMBE NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma kutoka kijiji cha Kanitelele
mkoani Njombe ikicheza ngoma ya Limdoya wakati alipowasili kwenye
kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe
Januari 25, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole
Sendeka.
Wasanii
kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe wakicheza ngoma ya Limdoya
wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye kiwanda cha chai
cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wanyakazi Januari 25, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha
chai cha Lupembe, Mussa Kefa (kushoto kwake) wakati alipotembelea
kiwanda hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon
Luhanjo wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua
kiwanda na kuzungumza na wafanyakazi akiwa katika ziara ya mkoa wa
Njombe Januari 25, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha chai
cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)