Posts

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHAI CHA LUPEMBE NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe ikicheza ngoma ya Limdoya wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. Wasanii kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe wakicheza ngoma ya Limdoya wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wanyakazi Januari 25, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha chai cha Lupembe, Mussa Kefa (kushoto kwake) wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wafanyakazi akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. 

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI AWAMU YA KWANZA YA MIUNDOMBINU NA UTOAJI HUDUMA YA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe

DADA HUYU AJIRUSHA KWENYE GOROFA BAADA YA KUGUNDUA MUME WAKE KAMPA MIMBA MAMA YAKE MZAZI

Image
VERY SAD NEWS!! Lady Commits Suicide After Catching Her Mother Sleeping With Her Husband!! According to Ghana news this lady commits suicide after catching her mother in relationship with her Husband also found out her mother was pregnant for her husband. This shocking revelation drove her mad instantly as she decided to jump from their apartment which was on a 30 store building. credit source:   report Ghana news

MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

Image
  Na Woinde Shizza,Arusha Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao. Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya . Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani. Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shaur

BREAKING NEWS : RAIS WA MAREKANI TRUMP AFUTA UFADHILI KWA MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA

Image
Donald Trump amerejesha utekelezwaji wa Sera ya Jiji la Mexico Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku kutolewa kwa pesa za serikali ya Marekani kufadhili mashirika ya nchi za nje ambayo yanatekeleza au kutoa habari kuhusu utoaji mimba.Afisa wake wa mawasiliano Sean Spicer amesema hatua hiyo ya rais inaonesha kwamba "anataka kuwatetea Wamarekani wote, wakiwemo wale ambao hawajazaliwa." Agizo hilo ambalo kirasmi linafahamika kama "the Mexico City Policy" (Sera ya Jiji la Mexico) huenda likayakera makundi ya kutetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na msimamo wake wa kupinga utoaji mimba.Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba upigwe marufuku Marekani.Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku dhidi ya ufadhili wa mashirika ya utoaji mimba nje ya Marekani kutolewa.Rais wa Republican Ronald Reagan mara ya kwanza alianzisha Sera ya Jiji la Mexico mwaka 1984 na k

AJALI YA BASI LA KIMBILINYIKO NA GARI DOGO YAPOTEZA MAISHA YA MTU MMOJA

Image
Basi la abiria mali ya Kampuni ya Kimbilinyiko lenye namba za usajili T 440 DCW likiwa limegongana na Gari ndogo aina ya Nissan Hardbody pickup yenye namba za usajili SU 37965, katika ajali iloyotokea jana jioni eneo la Miseyu, Barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam. inadaiwa mtu mmoja alipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. chanzo cha ajali hakikuweza patikana kwa haraka.Picha na Josephat Mmbando. Gari hizo zinavyoonekana kufuatia ajali hiyo. Sehemu ya Mashuhuda pamoja na abiria waliokuwemo kwenye basi hilo.

CHECK MATUKIO YA UHARIBIFU YALIOFANYWA NA WAANDAMAJI WANAOMPINGA DONALD TRUMP

Image
Mpaka usiku wa January 20 2017 Mamlaka kwenye taifa la Marekani zilisema wamekamatwa zaidi ya Waandamanaji mia moja (100) waliondamana kumpinga Rais mpya wa taifa hilo Donald Trump. Maandamano yalisikika sana kwenye mji wa Washington DC alikoapishwa Donald Trump lakini baada yakasikika sehemu nyingine kama Austin Texas ambako wameandamana pia vilevile lakini hizi hapa chini ni picha kutoka Washington DC na zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari. Mpaka gari la Polisi limevunjwa kioo cha nyuma Gari hili la kifahari lilichomwa moto ambapo Polisi na fire walipofika kwenye eneo la tukio walikuta tayari limewaka. Waandamanaji wengine walionekana wakivunja vioo vya magari na maduka kwenye mitaa ya Washington DC.

MSANII NUH MZIWANDA AFUNGUKA MENGINE KUHUSU SHILOLE

Image
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo. Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana. “Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana. Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.

JAJI CHANDE: NAFURAHI KUUACHA MUHIMILI WA MAHAKAMA KATIKA HALI NZURI

Image
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamedi Othman Chande amezitaka mahakama kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya awamu ya tano pamoja na kufuata maadili ya taaluma ya sheria katika kutoa haki na sawa kwa wakati na kwa watanzania wote. Jaji Mkuu Mstaafu - Mohamed Chande Othman Jaji Chande ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma ambapo amesema kuwa kuongezeka kwa uwazi katika shughuli za mahakama kutasaidia sana katika kuendeshwa kwa kesi na kuamuliwa kwa wakati na watendaji wake. Amesema anafurahi anauacha muhimili wa mahakama katika hali nzuri huku akiwataka watendaji kuendeleza juhudi za kuboresha mifumo taratibu na sheria ili kutoa nafasi zaidi kwa kesi nyingi kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo usikilizwaji wa kesi. Akizungumzia kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao ameuacha amesema kuendelezwa kwa mpango huo kutasaidia kuharakisha usikilizaji wa kesi, kuongeza mfumo wa usikilizwaji wa kesi pamoj

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA PROFESA IBREAHIM HAMISI JUMA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika

SABABU ZA EDWARD LOWASSA KUKAMATWA NA POLISI JANA

Image
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali.  Lowassa, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alikuwa njiani akitokea mkoani Kagera, ikiwa ni mwendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho katika kanda zake kutekeleza Operesheni Kata Funua inayohusisha mikutano ya ndani. Hata hivyo, aliachiwa jana jioni.   Akiwa ameongozana na viongozi na makada wa Chadema, Lowassa aliingia Geita saa 9:30 alasiri na kupokewa na umati wa wananchi waliojitokeza eneo la Nyankumbu, tayari kwa safari ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nkome.  Viongozi wengine waliokuwamo kwenye msafara huo ni Profesa Mwesiga Baregu, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Hamis Mgeja, ambaye ni kada wa chama hicho.  Msafara huo uliokuwa wa magari matano, ukisindikizwa na pikipiki na wafuasi kadhaa wa chama hicho, ulipitia makutano ya barabara

WAZIRI SIMBACHAWENE: “RUKSA WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA KUTUMIA MIHURI

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa muda kwa waraka uliotoa muungozo wa matumizi ya Mihuri kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji leo jijini Dar es Salaam. Na Beatrice Lyimo-MAELEZOSerikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya kuhudumia wananchi.Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.Mhe.Simbachawene alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali na watendaji wake wa chini.“Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya

Emmanuel Mbasha asema bado anamuhitaji mke wake Flora ingawa anadai amezaa nje ya ndoa

Image
Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na mwanaume mwingine. Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo. “Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.. “Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza. Muimbaji h