SABABU ZA EDWARD LOWASSA KUKAMATWA NA POLISI JANA
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali.
Akiwa
ameongozana na viongozi na makada wa Chadema, Lowassa aliingia Geita
saa 9:30 alasiri na kupokewa na umati wa wananchi waliojitokeza eneo la
Nyankumbu, tayari kwa safari ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa
kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nkome.
Viongozi
wengine waliokuwamo kwenye msafara huo ni Profesa Mwesiga Baregu,
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Hamis Mgeja, ambaye ni
kada wa chama hicho.
Msafara
huo uliokuwa wa magari matano, ukisindikizwa na pikipiki na wafuasi
kadhaa wa chama hicho, ulipitia makutano ya barabara mjini Geita na
kukutana na magari ya polisi yaliyosheheni askari wakiongozwa na Kamanda
wa Polisi wa Wilaya (OCD), Ally Kitumbo.
Bila kuingilia msafara huo, magari ya polisi yaliufuatilia kwa nyuma ulipokuwa ukielekea Kata ya Nkome.
Hali
ya hewa ilichafuka baada ya msafara kufika eneo la Soko Kuu wakati
wananchi walipouzuia wakitaka kumsalimia Lowassa, ambaye aligombea urais
katika uchaguzi mkuu uliopita.
Kiongozi
huyo alilazimika kujitokeza juu ya gari lake kuwapungia na baada ya
kelele za ‘njaa, njaa, njaa’ kusikika eneo hilo, Lowassa alitumia kipaza
sauti kuwaomba wananchi wawe watulivu na wawaruhusu waendelee na safari
yao kuwahi mkutano wa kampeni.
“Ndugu
zangu wana-Geita, natamani kuzungumza nanyi lakini sheria inanibana.
Naomba muwe watulivu na mturuhusu tuendelee na msafara kuwahi mkutano wa
kampeni Nkome,” alisema Lowassa.
Askari
hao wakiongozwa na OCD, walimfuata Lowassa na kumuamuru yeye na msafara
wake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano. Wakati wa kuelekea
kituoni, gari lake lilitanguliwa mbele na la polisi na nyuma kulikuwa na
jingine la jeshi hilo.
Kitendo
hicho kiliwafanya wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi
huyo kuongozana kwenda kituoni, jambo lililoibua taharuki na polisi
kuwatawanya kwa kufyatua mabomu ya machozi.
Waandishi wapigwa
Pamoja
na kuwatawanya wananchi kwa mabomu, askari hao pia waliwapiga kwa
mikanda na fimbo waandishi wa habari waliokuwa wakifanya kazi yao eneo
hilo.
Hali ilivyokuwa kituoni
Baada
ya kuwasili kituoni huku polisi wakiendelea kuwazuia wananchi, Lowassa
alisalia ndani ya gari lake hadi hali ilipotulia na kutakiwa kuingia
kituoni.
Ni
magari mawili pekee; la Lowassa na la Profesa Baregu, yaliyoruhusiwa
kuingia eneo la polisi huku viongozi wengine kama Singo Benson ambaye ni
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, na Upendo Peneza
(Mbunge wa Viti Maalumu), wakitakiwa kusubiri nje.
Kitendo
cha wananchi kuzidi kufurika kituoni hapo, kiliwafanya polisi
kuimarisha ulinzi, wakizuia mtu yeyote kukatiza wala kusogelea eneo
hilo. Licha ya kuzingira kituo cha polisi, askari walitanda barabara
inayoelekea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambako pia wananchi
walizuiwa kukatiza.
Lowassa apitishwa uani
Baada
ya kuona wananchi wanazidi kujaa kituoni, polisi waliamua kumtoa
Lowassa kupitia mlango wa nyuma na kumhamishia ofisini kwa Kamanda wa
Polisi wa Mkoa, Mponjoli Mwabulambo.
Kama
ilivyokuwa Kituo cha Kikuu cha Polisi, ulinzi pia uliimarishwa eneo
lote la ofisi ya RPC baada ya Lowassa kuhamishiwa huko na wananchi
kupata taarifa.
Kiongozi
huyo aliyehamia Chadema akitokea CCM mwaka 2015 aliachiwa jana jioni.
Kamanda Mwabulambo alisema hawakumkamata bali walizuia msafara huo kwa
ajili ya usalama wake.
Akizungumzia
suala hilo, Peneza alisema huo ni muendelezo wa ukandamizaji dhidi ya
viongozi wa Chadema unaofanywa na polisi mkoani Geita, akitoa mfano
kitendo cha yeye kuhojiwa kwa saa kadhaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa
madai ya uchochezi alipohutubia mkutano wa hadhara na kusema nchi
inakabiliwa na njaa.
Comments
Post a Comment