Emmanuel Mbasha asema bado anamuhitaji mke wake Flora ingawa anadai amezaa nje ya ndoa
Msanii
wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa
mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na
mwanaume mwingine.
Muimbaji
huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi
cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo.
“Moyo
wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea
2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na
maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha.
Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu
lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye
kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia
kipindi cha Enewz cha EATV..
“Mimi
sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto
labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi
nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza.
Muimbaji huyo alishinda kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya Mahakama kuthibitisha muimbaji huyo hakuwa na hatia.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mke wake huyo akimtuhumu aliyekuwa mume wake huyo kumbaka binti yatima ambaye walikuwa wanaishi naye.
Comments
Post a Comment