WAZIRI SIMBACHAWENE: “RUKSA WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA KUTUMIA MIHURI
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa muda kwa waraka
uliotoa muungozo wa matumizi ya Mihuri kwa Wenyeviti wa Serikali za
Mitaa na Vijiji leo jijini Dar es Salaam.
Na
Beatrice Lyimo-MAELEZOSerikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa
kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale
itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya
kuhudumia wananchi.Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa
kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.Mhe.Simbachawene alisema kuwa
nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali
na watendaji wake wa chini.“Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale
Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri
hiyo baada ya kujadiliwa na kushirikiana vya kutosha” alifafanua Waziri
Simbachawene.Mhe.Simbachawene alisema kuwa kuna baadhi ya wenyeviti wa
mitaa wamekuwa wakitumia vibaya mihuri hiyo na kupelekea migongano na
migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa ikiwemo maeneo ya Ununio,
Temeke.
Mbali na
hayo alisema kuwa katika Tangazo la Serikali namba 3 lililotolewa 5
Septemba, 1994 limeeleza baadhi ya vitendea kazi vya mwenyekiti wa mtaa
ni bendera yenye nembo ya Halmashauri, daftari ya kutunza kumbukumbu na
rejista ya makazi.Alisema kuwa mamlaka ya mwenyekiti haitokani na
mihuri, bali utendaji uliopo ndani ya mtaa au kijiji husika, hivyo
mamlaka ya mwenyekiti ipo pale pale na haibemwi na muhuri bali muhuri
huonesha nguvu ya ofisi baada ya kuwashirikisha watendaji tofauti ndani
ya kijiji katika kutoa maamuzi.
“Mhuri si
mali ya mwenyekiti binafsi, hivyo kwa yeyote atakayekiuka matumizi ya
mihuri hiyo Sheria itachukua mkondo wake” alisisitiza Mhe.
Simbachawene.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za
Mitaa Wilaya ya Temeke Bakiri Makele, ameahidi kushirikiana na Serikali
kwa kutumia mihuri hiyo kwa kufuata Sheria na taraibu zilizopo.Naye
Katibu wa Wenyeviti hao, Marium Machicha alimshukuru Waziri mwenye
dhamana kwa kauli aliyoitoa baada ya kuliona tatizo hilo na kuahidi
kulifanyia kazi.
Serikali
ilitoa Muongozo huo wa namna wa matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa
mitaa na vijiji kwa sababu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa baadhi ya
wenyeviti wa mtaa na vijiji nchini.
Comments
Post a Comment